DC KISHAPU AAGIZA MADIWANI KWENDA KUHIMIZA KULIMA MAZAO YANAYOSITAHIMILI UKAME, AZUNGUMZIA MAPATO NA WATUMISHI KUWA NA NIDHAMU


Madiwani wa halmashauri ya kishapu wakiwa kwenye kikao  cha baraza lao

Suzy Butondo, Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi amewaagiza madiwani wa halmashauri ya Kishapu na wataalamu kwenda kuwahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame na yanayoweza kuwalipa kwa wakati.

Hayo ameyasema leo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya pili kilicholenga kujadili taarifa za kata ambapo amesema asilimia 80 ya wananchi wa Kishapu wanategemea kilimo hivyo madiwani na wataalamu wakawahimize kulima mazao yanayostahimili ukame.

Amesema wakilima mazao yanayostahimili ukame hawatatumia nguvu kubwa, hivyo ni vizuri wahakikishe wanalima pamba na mazao mengine yanayostahimili ukame na wahakikishe wataalamu mbalimbali wa kilimo wanawafikia wakulima wote na kuwaelimisha wapande kisasa ili wapate kipato kikubwa, kwani wakiwa hawana kitu hata halmashauri itakuwa haina kitu.

Masindi akizungumzia suala la mapato, amewahimiza wataalamu na madiwani kudhibiti fedha kuanzia shilingi mbilimbli wanazozipata ili waweze kuzipeleka kwenye shughuli za maendeleo,

" Hakuna kitu kizuri na hakuna mtu mkarimu kama aliye na kipato kizuri, kwani ukiwa huna fedha muda mwingi unakuwa na hasira, hivyo tujitahidi sana kwenye suala la mapato tuhakikishe shilingi moja tunadhibiti, kwani hakuna milioni moja inayotoka hewani bila kuanza na shilingi moja, hivyo niwahimize kukusanya mapato kwa bidii "amesema Masindi.

Pia aliwataka watumishi wote kuwa na nidhamu wanapoitwa kuja kujibu hoja mbalimbali kwenye kikao cha baraza waje watoe ushikiano wa kujibu yanayotakiwa kujibiwa kwa wakati huo.

" Niwaombe sana watumishi wote umma muwe na nidhamu kwa sababu sisi watumishi wa umma tunatakiwa kuwa na nidhamu, na shughuli zote za umma tuzifanye kwa nidhamu na tutoe taarifa zilizonyooka, ukishaambiwa njoo utoe taarifa hii njoo utoe taarifa sahihi, kwani diwani yeyote akiongea hapa anamwakilisha mwananchi, na diwani akiondoka hapa atazungumzia miradi yote ya maendeleo na kutatua kero mbalimbali"amesema Masindi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wiaya ya Shinyanga Pita Mashenji amewataka waende wakasimamie utekelezaji wa ilani ya CCM, kwani kuna miradi mbalimbali bado haijatelkelezwa,hivyo aliomba kufikia mwezi wa tano iwe imekamilika yote.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson amesema maagizo yote yaliyotolewa kwenye kikao hicho wameyapokea na watayafanyia kazi ili na kuwataka watumidhi wote wafanye kazi bila kutoa visingizio.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Francis Manyanda amehimiza wataalamu wote kufanya kazi, na madiwani wote wakasimamie pale ambapo hapajamalizika, kwani kazi ya watumishi na madiwani ni kuhakikisha wanaitengeneza Kishapu ya Kesho.

Baadhi ya madiwani walitaja changamoto mbalimbali ambazo hazijatekelezwa katika maeneo yao ikiwemo maji umeme na miundombinu za barabara ambapo waliomba mamlaka husika zitekeleze kwa wakati ili kuondokana na kero hizo
AMakamo Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu Frances Manyanda akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Kishapu
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonhson akijibu hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akixungumza kwenye baraza hilo
Katibu wa chama cha mapinfuzi CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji akizungumza
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani humo wakiendelea kujafili hoja mbalimbali za maendeleo
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani humo wakiendelea kujafili hoja mbalimbali za maendeleo
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani humo wakiendelea kujafili hoja mbalimbali za maendeleo
Watumishi wa halmashauri hiyo na kamati ya usalama wakiwa kwenye kikao hicho
Watumishi wa halmashauri hiyo na kamati ya usalama wakiwa kwenye kikao hicho

























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464