KATIBU WA CCM WILAYA AWATAKA MAKATIBU JUMUIYA YA WAZAZI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO NA KUDUMISHA MSHIKAMANO

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha akizungumza na makatibu wa jumuiya wazazi kata na matawi

Na Suzy Butondo, Shinyanga

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha amewataka makatibu kata na wa matawi wa jumuiya ya wazazi watekeleze majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kudumisha upendo na mshikamano.

Hayo ameyasema leo wakati i akizungumza na viongozi hao kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kusajili wanachama kwani bado wanachama wengi hawajasajiliwa katika matawi mbalimbali.

Hamisa amesema makatibu wote wa Jumuiya ya wazazi wanatakiwa kutekeleza majukumu yao, ili kuhakikisha majukumu yote ya kata na wilaya yanatekelezeka kwa wakati .

"Hiki kikao ni cha kukumbushana ili muendelee kutekeleza majukumu yenu ya kazi na mkifanya hivyo mtaonekana chombo imara katika kuimarisha jumuiya na Chama, kwani nyinyi ndio injini inayotegemewa kwenye jumuiya na chama, pia naomba niwasihi makatibu wenzangu tushikamane tupendane, kwani katibu ni kiungo imara ambaye atamshauri vizuri mwenyekiti wake" amesema Chacha.

Aidha katibu Chacha amewataka wahakikishe malezi bora kwa watoto, kwani ni jukumu la wazazi kuonyesha malezi, "nendeni mkajipange kusajili wanachama , na mnaposikia kuna ziara yoyote ya viongozi, sherehe za jumuiya na Chama mjitokeze , na mshirikiane kwa pamoja ili kufanikisha jambo"

"Muendelee kuhakikisha mnashiriki maadhimisho yote ya jumuiya na Chama Cha Mapinduzi, lakini pia niwaombe kila katibu ahakikishe anatekeleza jukumu lake kila baada ya miezi mitatu vikao vya kikanuni vifanyike kwa wakati, pia tuanze kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi na tuwaunge mkono viongozi walioko madarakani na tushirikiane na wenyeviti wetu wa serikali za mitaa."amesema.

Kwa upande wake Katibu wa Wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Doris Kibabi aliagiza kila shina na matawi kusajili wanachama wote ambao hawajasajiliwa, na kila katibu afanye kazi hiyo ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa asilimia 100.

"Tumewaita hapa kwa lengo la kuwataka mkafanye usajili ili kujua idadi ya wanachama wetu, hivyo makatibu wote twendeni tukajipange kusajili wanachama kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanachama wote wamesajiliwa" amesema Kibabi.

"Kuna baadhi ya makatibu wameanza kuwamegua viongozi na kuweka wake  au ndugu zao kwenye kamati za utekelezaji baada ya kusikia maelekezo ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu kuwa watashiriki kwenye mkutano mkuu, hili suala sitaliruhusu kwani ninayo majina ya viongozi waliochaguliwa, watakao waleta watawatafutia sehemu ya kuwaweka"ameongeza Kibabi.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya Fue Mrindoko amewataka makatibu wazingatie maagizo yote waliyopewa na kuhakikisha jumuiya ya wazazi inakuwa imara nakushirikiana na viongozi wote wa CCM.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Hamisa Chacha akizungumza na makatibu wa jumuiya ya wazazi kata na Matawi wa wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wlaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindiko akizungumza na makatibu wa Jumuiya ya wazazi kata na matawi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wlaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindiko akizungumza na makatibu wa Jumuiya ya wazazi kata na matawi
Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi akizungumza na makatibu wa Jumuiya ya wazazi kata na matawi

Makatibu kata na matawi wa jumuiya ya wazazi wakimsikiliza katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha akizungumza

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464