Suzy Butondo, Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye ni naibu waziri, ofisi ya waziri mkuu kazi vijana, ajira na wenye ulemavu leo ameeleza Taarifa yake ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo la Shinyanga , uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.
Akieleza kwenye mkutano mkuu wa CCM jimbo la Shinyanga mjini uliofanyika mjini hapa, ambapo mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa katibu mkuu wazazi Taifa Ally Hapi, ambapo amesema kupitia ilani ya Chama cha mapinduzi CCM ametekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, barabara, maji masoko, na umeme, ameboresha kwa kuhakikisha miundombinu inapitika ipasavyo.
"Katika sekta ya elimu ameboresha miundombinu ya madarasa imeongezeka ikiwemo madawati na vifaa mbalimbali kwa ajili ya elimu, katika sekta ya afya ameborsha kwa kuleta vifaa mbalimbali yakiwemo magari ya kuwahisha wagonjwa kupata huduma za matibabu ambazo nimeleta magari sita kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Shinyanga"amesema Katambi.
"Hivyo tunampongeza mama yetu mama Samia Suluhu kwa kuendelea kutujali pale tunapompelekea kero mbalimbali anajali wananchi wakehataki wapate shida, ndiyomaana anatoa fedha nyingi kwa ajiliya kuondoa changamoto mbalimbali katika jimbo la Shinyanga na mkoa kwa ujumla" ameongeza Katambi.
"Samia huyu huyu ameleta mabadiliko makubwa katika jimbo la Shinyanga, mkoa na nchi nzima amefanya makubwa, ambayo hayawezi kuelezeka, kwa kweli kama kuupiga mwingi mama ameupiga anatupenda watanzani hataki wananchi wake wapate shida
Aidha amewapongeza madiwani wote wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mjini kwa kutoa ushirikiano kwa ajili ya kufanya maendeleo, hali ambayo imekuwa ikisaidia kuondoa changamoto mbalimbali katika kata na wilaya.
Hata hivyo ameomba barabara ya kwenda Mwawaza katika hospitali ya rufaa ya mkoa iwekwe kwenye bajeti ili kina mama wajawazito na wagonjwa wanaokwenda kupata huduma wasipate shida, ikiwa ni pamoja na kupunguza vumbi kwa wananchi wanaoishi Ndala.
"Niombe endeleeni kuwaheshimu madiwani wote wa manispaa ya Shinyanga, tudigombane tukigombana tutapoteza madiwani wetu wengi, tusikubali kugombanishwa na watu tufanyeni kazi kwa kushurikiana hatuna sababu ya kugombana, ili katika uchaguzi wetu mkuutupate kura nyingizaidi" amesema Katambi
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo amesema anamhakikishia katibu wa wazazi Taifa kwamba katika uchaguzi mkuu wanaenda kushinda kwa kishindo kikubwa, pia amempongeza mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa kufanya kazi kubwa ya maendeleo.
"Endelea kupambana kweli wewe ni mchapa kazi kwa kushirikiana na mama yetu mama Samia Suluhu mmefanya kazi kubwa sana, hivyo niwaombe wajumbe mwacheni Katambi afanye kazi, acheni kuvunja kanuni na sheria, tuziheshimukanuni tuheshimu katiba shirikianeni na mbunge wenu katika kuleta maendeleo,"amesema Odilia.
"Pia tusisahau kwamba mgombea wetu wa Urais ni Samia Suluhu Hasan, hivyo twendeni tukamuunge mkono ili ashinde kwa kishindo kwa asilimia 100" ameongeza
Wajumbe wa mkutano mkuu wakimsikiliza Mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi
Wajumbe wa mkutano mkuu wakimsikiliza Mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi