Na Mwandishi wetu - Dodoma
Uongozi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA -TAN )umefanya ziara ya kujenga mahusiano kwenye Makao Makuu ya Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa PSSSF Jijini Dodoma na kujionea ufanisi wa mfuko huo katika kuwahudumia Watanzania.
Mwenyekiti wa MISA TAN. Bwana Edwin Soko alisema lengo kuu la ziara hiyo ni uongozi mpya wa MISA Tan kujitambulisha kwa PSSSF ili kuongeza mahusiano na mfuko huo pamoja na kuona utendaji wa mfuko huo kwa kuwa waandishi wa habari Tanzania ni wanafaika wa mfuko huo na ni mabalozi wazuri wa shughuli za PSSSF. wakiwemo wanachama wa MISA TAN.
"Nimejifunza mengi Kwa kutembelea Idara mbalimbali ndani ya PSSSF kama vile idara ya kupokea simu Kwa wateja(Call Centre), Idara ya huduma Kwa wateja, Idara ya mafao Kwa wateja na Idara ya utunzaji wa taarifa za wanachama, huko kote nimeona umahiri wa wafanyakazi wa PSSSF kwenye kutoa huduma Kwa watanzania", alisema Soko.
Pia Bwana Soko alimpongeza Mkurugenzi wa PSSSF Bwana Abdul-Razak Badru Idara nzima ya Mahusiano na Elimu Kwa umma kwa kufanya kazi vizuri hususani kwenye kuwa kiungo muhimu katika kutoa taarifa za huduma mbalimbali za PSSSF kwa vyombo vya habari Nchini ili kuwapa nafasi watanzania kupima ufanisi wa Mfuko huo.
Naye Bibi Regina Kumba Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF alieleza kuwa majukumu makubwa ya PSSSF ni kusajiri wanachama, kukusanya michango , kuwekeza na kutoa mafao Kwa wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF kupitia mafao ya ya muda mrefu kama vile mafao ya uzeeni, mafao ya ulemavu, mafao ya kifo na mafao ya wategemezi.
Pia Bibi Kumba alieleza pia mafao ya muda mfupi yakiwemo , mafao ya kukosa ajira, na mafao ya uzazi.
Bibi Kumba alieleza kuwa, PSSF inafanya kazi kwa katika Kanda mbalimbali Kwa kutumia mifumo ya kisasa ya utunzaji wa kumbukumbu za wanachama Kwa lengo la kuboresha mahusiano na wateja wote wa PSSSF.
Kwa pamoja uongozi wa MISA Tan na idara ya Mahusiano na Elimu kwa Umma zimekubaliana kuendelea kushirikiana kwenye kufanya kazi kwa pamoja ikiwemo kuhamasisha waandishi wa habari kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya PSSSF pamoja na kuwa mabalozi wa wazuri wa PSSSF ili kujenga Leo yetu na kesho yetu Kwa pamoja.