Shirika lisilo la kiserikali la Youth and Women Emancipation (YAWE) linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia, ulinzi wa Mtoto, Afya na Lishe, Mazingira na mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na Demokrasia na Utawala Bora upande wa maendeleo ya jamii kwa njia ya kuwahamasisha vijana kushiriki shughuli za kiuchumi katika jamii limwewajengea uwezo vijana wa kike na wa kiume wa Manispaa ya Shinyanga kushiriki katika afua za upangaji wa bajeti kuanzia ngazi ya serikali za mitaa, manispaa na serikali kuu.
Vijana hao wakiwemo wenye ulemavu ambao wanatekeleza mradi wa kupanda miti na utunzaji wa mazingira wa miezi takriban saba kwa wakiwezeshwa na shirika la YAWE wamesema ushirikishwaji mdogo wa vijana katika mipango ya bajeti za Serikali unasababisha shughuli nyingi za maendeleo zinazowahusu vijana kukwama ikiwa ni Pamoja na ukosefu wa ajira ali ambayo inaosababisha vijana wengi kuonekana wakirandaranda mitaani kushinda mitaani huku wengine wakizurura kwenye maofisi kutafuta kazi bila mafanikio.
Afisa Miradi wa Mapambano Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi wa Shirika la TYAWE, Peter Nampala amesema shirika limeona ni vyema kuwajengea uwezo vijana kwakuwa takwimu ya idadi ya watu kupitia sensa iliyopita imeonyesha kundi la vijani ni wengi zaidi kuliko makundi mengine hivyo Serikali haina budi kuweka kipaumbele kikubwa katika mauakla yanayowahusu vijana wa makundi yote wakiwemo walemavu.
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Pascal Iyela amesema mipango ya bajeti za Serikali zinapaswa kuwashirikisha watu wote wakiwemo vijana ambapo kwa ujumla wanatakiwa kushiriki kutoa maoni yako kupitia mikutano ya vijiji na njia nyingine ni kuwasilisha mapendekezo kupitia viongozi wa vitongoji, vijiji na kata ambapo mapendekezo yao ya vipaumbele yatawasilishwa katika ngazi husika ili kuingizwa kwenye bajeti husika.
Afisa Miradi wa Shirika Peter Nampala akitoa ufafanuzi wa mafunzo ya Ushiriki wa Vijana kwenye mipango ya bajeti za Serikali
Mchumi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pascal Iyela akitoa mada ya ushiriki wa Vijana katika mipango ya Bajeti za Serikali
Vijana wakiendelea kuzikiliza mada ya ushiriki na ushirikishwaji kwenye mipango ya bajeti za Serikali
Mada ikiendelea kuhusu Vijana kushiriki kwenye mipango ya bajeti za Serikali
Vijana wakiendelea na majadiliano baada ya mafunzo ya ushiriki na ushirikishwaji wa mipango ya bajeti za Serikali