MWENYEKITI WA UWT MKOA WA SHINYANGA AHIMIZA UPENDO NA MSHIKAMANO KWA VIONGOZI

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini

Suzy Butondo, Shinyanga

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samweli Bizuri amewataka viongozi wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini kupendana na kushirikiana katika kufanya shughuli mbalimbali za kuweza kukijenga chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Jumuia zake ili kuhakikisha katika uchaguzi wanapata kura nyingi kwa madiwani na wabunge.

Hayo ameyasema kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini, ambapo pia aliwapongeza wanawake kwa kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi za serikali za mitaa na kupata ushindi wa asilimia 99.

“Nawapongeza sana viongozi wote wa UWT Shinyanga mjini kwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika chaguzi za serikali za mitaa, niwaombe muendelee kupendana na kushirikiana, pale mnapokutana na changamoto muwaone viongozi wenu wa ngazi za juu waweze kuwasaidia”amesema Bizuri.

Kwa upande wake katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga … aliwatakia viongozi pamoja na madiwani wasimamie zoezi la usajili ili kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika mfumo wa kidigitali, kwani kuna baadhi ya wanachama bado hawajasajiliwa.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewapongeza makatibu wa UWT wenyeviti wa matawi na kata zote, madiwani na wajumbe wote wa Baraza wilaya kwa kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwataka waenelee kushikama hivyo hivyo siku zote.

Aidha katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Geturude Mboyi amewaomba viongozi wote wa UWT wilaya wanapoendelea kufanya kazi za kujenga umoja wao na chama wahakikishe wanatunza siri ili kuhakikisha usalama wa kazi zao.

















































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464