MAKOMBE AZINDUA KITUO CHA MAAFISA USAFIRISHAJI “BODABODA” MAJENGO MAPYA SOKONI
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe,amezindua kituo cha maafisa usafrishaji “Bodaboda” cha Majengo Mapya Sokoni,huku akiwaonya wasitongoze wake za watu,wanafunzi, na kuwasihi watii sheria za usalama barabarani.
Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 3,2025 katika Kituo hicho cha Bodaboda Majengo Mapya,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Makombe akizungumza wakati wa kuzindua Kituo hicho, amewapongeza vijana hao kwa kujiajiri wenyewe na kuendesha maisha yao, huku akiwasihi katika shughuli zao hizo za usafirishaji wawe na maadili na kuacha kutongoza wake za watu, wakiwamo na wanafunzi kutogeuza wake zao,ili kituo hicho kiwe cha mfano kwa bodaboda wote.
“Kituo hiki cha Bodaboda kimezinduliwa na CCM hivyo tunataka kiwe cha mfano kwa bodaboda wote,kuweni na maadili mema msivunje ndoa za watu,msigeuze wanafunzi kuwa wake zenu na pia mtii sheria za usalama barabara ili mnapoendesha pikipiki zenu muwe salama,”amesema Makombe.
Aidha,akijibu maombi ya vijana hao juu ya mikopo ya pikipiki, amewahidi kwamba tatizo lao litashughulikiwa sababu ilani ya CCM inatamka juu ya kusaidia vijana,huku akiwasihi waendelee kujiunga kwenye vikundi vya vijana, ili wapate mikopo ya halmashauri asilimia 10 ambayo 4 hutolewa kwa vijana.
Pia,amewasihi vijana hao kwamba waendelee kusomea mafunzo ya udereva kama ambavyo wanaendelea kufanya kwenye kikundi hicho kwa kupeleka baadhi ya vijana kusomea udereva ili wajue sheria za usalama barabarani,na kwamba pia kuna fursa ya kusoma fursa mbalimbali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katika hatua nyingine,amewaomba wananchi waendelee kukiamini Chama cha Mapinduzi (CCM),ili kiendelee kushika dola na kuendelea kuwaletea maendeleo pamoja na kutatua matatizo yao.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha, amepinga vikali baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidharua kazi ya Bodaboda, na kubainisha kwamba kazi hiyo ni kama kazi nyingine,na ndiyo maana serikali ilitoa fursa ya kurahisisha usafirishaji.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,amewasihi vijana waendelee kuchangamkia fursa za mikopo ya halmashauri kupitia kwa maafisa maendeleo kwenye Kata zao, ili wapate mikopo na kujikwamua kiuchumi.
Mjumbe wa kikundi hicho Elias Kamuga,akisoma taarifa ya amesema kikundi chao kinazaidi ya miaka mitano na walianza wakiwa watu 7,lakini sasa hivi wamefika 45 na wamekuwa wakipeleka baadhi ya vijana kusoma mafunzo ya udereva.
Amesema kati ya vijana hao 45, tayari wameshaunda kikundi cha watu Watano kwa ajili ya kuomba mkopo,huku wakiomba pia kusaidiwa kupata mikopo ya Pikipiki.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizungumza wakati wa kizundua Kituo cha Maafisa usafirishaji "Bodaboda"cha Majengo Mapya Sokoni Kata ya Ngokolo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akizundua Kituo cha Bodaboda Majengo Mapya Sokoni.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza kwenye uzinduzi huo wa Kituo cha Bodaboda.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo hicho cha Bodaboda.
Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini Fuel Mlindoko akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo hicho cha Bodaboda.
Elias Kamuga akisoma taarifa ya kituo hicho cha Bodaboda.
Uzinduzi wa Kituo cha Bodaboda Majengo Mapya Sokoni ukiendelea Kaya ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Kiapo cha kuunga Mkono adhimio la Mkutano Mkuu wa CCM kumpitisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea pekee wa Urais kupitia tiketi ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu 2025, na Mgombea mwenza Dk.Emmanuel Nchimbi pamoja na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi.
Maafisa usafirishaji "Bodaboda" Kituo cha Majengo Mapya Sokoni awakimsindika Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Mkombe kwa ajili ya kuzindua Kituo chao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464