MADIWANI SHYDC WAJADILI TAARIFA MBALIMBALI KIKAO CHA BARAZA,KWA MAENDELEO YA WANANCHI, HALMASHAURI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,wamejadili taarifa mbalimbali kwenye kikao cha baraza,kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya wananchi na halmashauri hiyo.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani kimefanyika leo Februari 5,2025 kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ngassa Mboje.
Madiwani hao wakijadili taarifa hizo,wamesisitiza kwamba maelekezo ambayo wamekuwa wakiyatoa kwa menejiment ya Halmashauri pamoja na taasisi za serikali, kwamba yazingatiwe ili kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi.
Wakichangia taarifa ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)wilaya ya Shinyanga,wamesema barabara nyingi wilayani humo ni mbovu sababu ya kuharibiwa na mvua, na kwamba katika utekelezaji wa miradi hiyo wawe wanashirikishwa viongozi wa maeneo husika wakiwamo Madiwani.
Mmoja wa Madiwani hao Diwani wa Lyamidati Veronica Mabeja, amesema barabara ya kutoka Mishepo-Lyamidati hadi Kizungu ni mbovu, na kuomba ifanyiwe matengenezo ya haraka.
Aidha, katika maswali ya papo kwa papo diwani wa Nyida Seleman Segereti, aliuliza swali juu ya hatua ambayo imechukua halmashauri kukusanya mapato katika machimbo mapya ya madini ya Almasi Kata ya Mwatini.
Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)wilaya ya Shinyanga Mhandisi Kulwa Awadhi, akijibu maswali ya madiwani, amesema barabara zote zitafanyiwa matengenezo awamu kwa awamu,huku zingine tayari Wakandarasi wapo “site” wakiendelea na utekelezaji.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, amewataka TARURA waendelee kutatua changamoto za ubovu wa miundombinu ya barabara wilayani humo, na kwamba zinapokuwa zinafanyiwa matengenezo washirikishwe pia viongozi wa maeneo husika wakiwamo madiwani.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela, naye amewasisitiza TARURA kwamba, wawe wanawafuatilia Wakandarasi wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo barabara, ili waikamilishe kwa wakati, pamoja na kujihakikisha kama kweli wapo eneo la mradi“site”.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Mtomela, akijibu maswali papo kwa pao juu ya ukusanyaji mapato kwenye Machimbo mapya ya Madini ya Almasi Mwantini, amesema tayari wameshaanza kukusanya mapato, na kwamba kati ya wafanyabiashara 66 tayari Sita wameshalipa mapato.
Akiwasilisha pia Taarifa ya Mkurugenzi kwenye Baraza hilo, amewasihi Madiwani kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao kujiandikisha shule katika masomo ya awali, na darasa la kwanza, pamoja na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wahudhulie shule sababu bado muitikio siyo mzuri.
Ametoa wito pia kwa wazazi na walezi,kwamba wawapeleke watoto wao shule, pamoja na watoto wenye ulemavu na siyo kuwaficha ili nao wapate haki yao ya elimu.
Amewasisitiza pia wananchi,kuwa zoezi la utoaji chanjo ya mifugo litakapofika, wawe na muitikio mkubwa ili mifugo yao ipate chanjo hiyo na kuwa salama ambapo kwa Ng’ombe mmoja itakuwa sh.500,Mbuzi 300.
Amempongeza pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa Gari jingine la Wagonjwa “Ambulance” wilayani humo, pamoja na Pikipiki 2 ambazo zinatasaidia katika utoaji wa huduma za chanjo.
Katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani ziliwasilishwa pia taarifa mbalimbali za Taasisi za Serikali ikiwamo ya RUWASA, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo tawi la Shinyanga,VETA, Tume ya Utumishi Walimu,pamoja na Taarifa mbalimbali za Kamati.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Mtomela akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Kikao Baraza la Madiwani kikiendelea.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Ras akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Afisa Tarafa ya Samuye Aaron Laizer akizungmza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani akiwasilisha Taarifa ya DC Julius Mtatiro.
Diwani wa Ilola Amos Mshandete akichangia mada kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga akiwasilisha taarifa kwenye Baraza la Madiwani.
Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Kulwa Awadhi akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha Baraza.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Diwani wa Lyamidati Veronica Mabeja akichangia mada kwenye kikao cha Baraza.
Baraza la Madiwani likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464