MISA TAN YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUONGOZA JUHUDI ZA SULUHU DRC

Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan) imetoa pongezi Kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali na watanzania wote Kwa kukubali kuwa Mwenyeji wa makutano wa kutafuta Suluhu ya hali ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Nchi ya Congo.

MISA Tanzania imesema kitendo hicho ni ishara ya upendo na uzalendo Kwa Bara Zima la Afrika.

Pia MISA imevitaka vyombo vya habari kote Afrika Mashariki, Kusini Mwa Afrika na Afrika Kwa ujumla kuzingatia weledi vinapoandika habari za mzozo wa DRC kwa kuwa taarifa zisizo sahihi zinaweza kuzidisha chuki Kwa Nchi zilizopo kwenye mzozo.

MISA imependekeza. Waandishi wa Habari watumie uandishi wa habari za kuleta suluhisho ( constructive Journalism) ili kuripoti Kwa kueleza ukweli katika mizania ya hasi na chana na Nini kifanyike.

Februari 8 siku ya jana Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Nchi za Kusini mwa Afrika walikutana na kufikia Maazimio mbalimbali yenye lengo la kusitisha vurugu zinazoendelea Mashariki ya DRC inayojumuisha mji wa Goma.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464