Na Suzy Butondo, Shinyanga
Katika kuadhimisha kwa miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu ameshirikiana na wanachama pamoja wananchi kupanda miti katika shule ya sekondari Ngokolo na katika uwanja wa Zahanati uliopo maeneo ya Mshikamano mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga.
Mkwizu amesema leo katika kata ya Nokolo wamehitimisha raimi maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kupanda miti katika shule ya Ngokolo Sekondari na katika kiwanja ambacho wanatarajia kujenga zahanati ya kata ya Ngokolo ulioko katika maeneo ya Mshikamano.
“Tulianza na Jumuiya yetu ya wazazi ambayo imepanda miti katika shule ya msingi Mwadui leo tumekuja kuhitimishia hapa kwa kupanda miti tunauomba uongozi wa shule uhakikishe miti hii inasimamiwa na kulinda mifugo wasiishambulie”,amesema Mkwizu.
“Hili eneo la Zahanati ni moja ya ahadi nilizoahidi wakati naomba kura kwa wananchi niliahidi kujenga soko tayari tuna masoko mazuri Majengo na mitumbani tumeboresha, na uwanja huu hivi karibuni tutaanza ujenzi ili kuhakikisha wananchi wa Ngokolo wanapata huduma hapa, kwani tayari ramani ya Majengo na mpango huu uko kwenye bajeti tayari kwa utekelezaji”,ameongea Mkwizu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Ngokolo Mwandu amesitiza viongozi wote ambao wameshiriki upandaji miti huo wasiache kusimamia miti ili mifugo wasishambulie, kwani kuna miti iliyopandwa awali ilishambuliwa na mifugo bila kujua ni mifugo wa nani, hivyo sasa hivi zitafuatwa sheria wanatakaoachia mifugo yao watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Naye mwalimu mkuu wa Shule ya sekondari Ngokolo James Msimba amesema anawashukuru wazazi kwa ushirikiano wao wa karibu na walimu kwani umezaa matunda watoto wamefaulu vizuri kwa asilimia kubwa, hivyo amewataka wazazi waendelee kuwasisitiza watoto wao wasome kwa bidii ili waweze kufaulu zaidi na tuendele na kampeni yetu ya tokomeza ziro mafanikio yanaonekana