KATAMBI APOKELEWA KIFALME MWAMALILI,WANANCHI WAKOSHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

KATAMBI APOKELEWA KIFALME MWAMALILI,WANANCHI WAKOSHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu,amepokelewa na wananchi wa Mwamalili kwa shangwe,wakieleza ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye Kata hiyo.
Katambi amewasili leo Februari 24,2025 kwenye Kata hiyo ya Mwamalil,ili kuzungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Mwalili,pamoja na kuwaeleza wananchi yale ambayo ameyatekeleza kwao ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge.

Awali akiwasili kwenye Mkutano,wananchi walimpokea Mbunge huyu na kisha kumbeba juu juu kama Mfalme wakieleza kuridhishwa na namna anavyochapa kazi katika kutatua shida na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwananchi Charles Dotto,amesema hawakuamini kama Mbunge huyo atawaletea maendeleo,sababu wamezoea watu wakipata Ubunge wanakwenda jumla,lakini Katambi yupo tofauti na anatekeleza kwa vitendo.

"Kwa kweli tumeridhiswa na utendaji kazi wa Katambi,Diwani wetu Matinde na Rais Samia miradi inaonekana,"amesema Dotto.
Diwani wa Mwamalili James Matinde alizungunza kwenye Mkutano huo, ametoa ushuhuda namna Mbunge Katambi anavyosikiliza shida za wananchi na kuzitatua.

Amesema kipindi anapiga Kampeni kwa wananchi kuomba kura aliahidi mambo makubwa,ikiwamo kuwapelekea huduma ya umeme na maji, na kwamba baada ya kupata udiwani akaona ahadi alizoahidi wananchi itakuwa ngumu kutekelezeka kutoka na majibu aliyopewa Halmashauri.
Anasema ilibidi amtafute Mbunge Katambi na kumueleza kero hizo za wananchi, ambapo alimsikiliza na kisha kuzitatua na sasa wananchi wana umeme na maji, na kumpongeza Mbunge huyo kwa kuguswa na matatizo ya wananchi.

"Katambi ni Mbunge ambaye anaguswa na Matatizo ya Watu Mwamalili haikuwa hivi, lakini ndani ya miaka Minne mmeona imebadilika kimaendelo, Barabara na Madaraja ambayo yalikuwa kero yamejengwa, na bado tunaendelea kukamilisha miradi mingine,"amesema Matinde.
Aidha, amesema kwa kipindi cha miaka Minne kuanzia 2020-2024 Miradi 21 ya Maendeleo imetekelezwa pamoja na kupokea kiasi cha fedha sh.bilioni 1.4 za maendeleo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye Kata hiyo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe,amesema Mbunge Katambi ameitendea haki ilani ya uchaguzi ya chama hicho kwa vitendo, sababu amekuwa akufuatilia fedha kupitia nafasi yake ya Naibu Waziri, na kisha Rais Samia anamsikiliza na kutoa pesa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Naye Mbunge Katambi, amesema yeye wakati akiomba kuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, alihidi kuwatumikia wananchi na ndiyo maana anapambana ili kuhakikisha ahadi zote ambazo aliahidi anazitekeleza.

Amesema yeye siyo Mbunge wa Starehe bali ni kutumikia wananchi na ndiyo maana anafanya ziara ya kuwaeleza nini ambacho amekifanya ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge licha ya kila mtu kujione mwenyewe kwa macho yake miradi ya maendeleo ambayo ameitekeleza.

Aidha,amewahidi pia wananchi kwamba kwa zile barabara ambazo zimeharibiwa na mvua tayari fedha zimeshapatikana sh.milioni 500 za kufanyia matengenezo na kwamba kuna fedha zingine zitakuja milioni 500 na kufika bilioni 1 za ukarabati, huku akiwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali yao chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan sababu ikiahidi inatekeleza.

Amesema kwamba kwa zile changamoto ambazo zimesalia kutekeleza zitakelezwa pamoja na ukamilishwaji wa jengo la Ofisi ya Kata Mwamalili kama diwani alivyoomba kuungwa mkono, pamoja na kusambaza huduma ya umeme kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa pamoja na maji.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464