UWT KATA YA NGOKOLO WATOA MSAADA KITUO CHA SHINYANGA SOCIETY ORPHANS


Mwenyekiti wa UWT kata ya Ngokolo Hulda Masaba akigawa zawadi hizo kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphans

Suzy Butondo, Shinyanga

Umoja wa Wanawake Tanzania UWT kata ya Ngokolo ukiongozwa na mwenyekiti wake Hulda Masaba umeadhimisha kuzaliwa kwa miaka 48 ya CCM kwa kutoa zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphans kilichopo maeneo ya Bushushu katika manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa UWT kata hiyo Hulda akikabidhi zawadi hizo amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuwakumbuka watoto hao, kwani wanajisikia vizuri wakiona wadau mbalimbali wakiwapa zawadi na misaada.

“Sisi wanawake wa Ngokolo katika kuadhimisha kwetu kwa kuzaliwa kwa miaka 48 ya CCM tumeona tuje tutoe zawadi kwa watoto wetu wanaolelewa katika kituo hiki ili nao waweze kuadhimisha nasi kuzaliwa kwa CCM”amesema Hulda.

Kwa upande wake diwani wa kata ya ngokolo ambaye aliambatana na UWT kwenda kutoa msaada huo amesema ameona aambatane na UWT kwenda kuwajulia hali watoto hao, amempongeza mkurugenzi wa kituo hicho kwa kuwalea vizuri na kuwaomba wadau mbalimbali kuwatembelea watoto hao na kuwajulia hali, kwani wanajisikia vizuri.

 Mkurugenzi wa kituo hicho Ayam Ally Said ameushukuru umoja huo kwa kutoa zawadi hizo “tunawashukuru sana kwa kuwakumbuka watoto wetu hawa tunawaombea kwa Mungu awabariki pale mlipotoa Mungu awaongezee”.
Mwenyekiti wa UWT kata ya Ngokolo Hulda Masaba akifurahi na watoto wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphans
Mwenyekiti wa UWT kata ya Ngokolo Hulda Masaba na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphans















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464