KATAMBI AANZA ZIARA KATA KWA KATA KUWAELEZA WANANCHI ALIYOYATEKELEZA NDANI YA MIAKA YAKE MINNE YA UBUNGE,AOMBA KURA NYINGI ZA RAIS SAMIA UCHAGUZI MKUU 2025

KATAMBI AANZA ZIARA KATA KWA KATA KUWAELEZA WANANCHI ALIYOYATEKELEZA NDANI YA MIAKA YAKE MINNE YA UBUNGE,AOMBA KURA NYINGI ZA RAIS SAMIA UCHAGUZI MKUU 2025

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, ameanza ziara yake ya kutembelea Kata kwa Kata kuwaeleza wananchi aliyoyatekeleza ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge, chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,na kumwombea katika uchaguzi mkuu 2025 wampigie kura nyingi za ushindi.
Ameanza ziara hiyo leo Februari 23,2025 kwa kuzungumza kwanza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Kizumbi na Ibinzamata kwenye vikao vya ndani, na kisha kufanya Mkutano wa Hadhara na Wananchi wa Kizumbi.

Katika mkutano huo amewaeleza wananchi kuwa, ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge, ameibadilisha Shinyanga kimaendeleo na ahadi nyingi ambazo aliahidi amezitekeleza,huku akimshukuru Rais Dk,Samia Suluhu Hassan kwa kumshika mkono sababu kila anachokiomba kwake anakitekeleza.
“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ni Mwadilifu,Mwaminifu, Mzalendo anayetekeleza, hivyo naombe mpigieni kura nyingi za ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, sababu Shinyanga mjini ameitendea haki, ndani ya miaka Minne ya Ubunge wangu imepiga hatua kubwa kimaendeleo na bado anazidi kumwaga pesa,”amesema Katambi.

Ametaja miradi ambayo ameitekeleza kila sekta, kwamba kwa upande wa Elimu kipindi anaingia kwenye Ubunge Shinyanga Mjini kulikuwa na shule 65 za Msingi na Sekondari, lakini wamejenga shule mpya 10 mpya na hivyo kufikisha shule 75, pamoja na kujengwa pia shule ya Wasichana ambayo haikuwepo,huku wakitatua pia tatizo la upungufu wa walimu kutoka 421 hadi 180.
Amesema pia wanapanua Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi hapa Shinyanga ambapo kimepatikana kiasi cha fedha sh,bilioni 11 kwa ajili ya kuongeza majengo ili kiwe na wanafunzi 3,000, pamoja na kuwepo na mikakati ya kupanua Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na pia wameleta Tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ili kuongeza mzunguko wa fedha.

Kwa upande wa miundombinu ya barabara, ametatua changamoto kwenye maeneo ambayo yalikuwa korofi, pamoja na kujenga madaraja, huku akimpongeza Rais Samia kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa barabara,ikiwamo na Barabara ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mwawaza kwa kiwango cha Lami.
Amezungumzia umeme kwamba maeneo mengi yamepelekewa huduma za umeme na kwamba kunapesa tena sh.bilioni 3 zimetolewa kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye maeneo ambayo hayana umeme, huku akiwataka TANESCO kwenye maeneo ambayo wamechimba mashimo na wawajaweka nguzo kwa kipindi kirefu ni vyema wafukie mashimo hayo, pamoja na maeneo yenye nguzo wafunge waya ili wananchi wapate huduma.

Kwa upande wa huduma ya maji, amesema maeneo mengi yamefikiwa na huduma hiyo, na kwamba kunafedha tena imepatikana Sh.bilioni 195 zipo Shuwasa, kwa ajili ya kusambaza zaidi mtandao wa maji kwa wananchi.

“kazi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani mwanamke ipo pale pale, ndiyo maana anatoa fedha na miradi mingi ya maji inazidi kutekelezwa,Mama ukimuomba anasikia na kutekeleza,”amesema Katambi.

Amegusia pia suala la Afya kwamba ndani ya Ubunge wake huduma za afya zimeimarika zaidi ikiwamo ujenzi wa Zahanati,Vituo vya Afya,upatikanaji wa vifaa tiba na madawa pamoja na ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na ya Mkoa.
Pia, amewasihi vijana kuchangakia fursa ya masomo bure ya kupata ujuzi ambayo yanafadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusoma bure katika Chuo cha Hillforest cha Shinyanga, ambapo wataweza kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha, amempongeza Mbunge kwa kuitendea haki ilani ya uchaguzi ya Chama hicho, ambapo ahadi ambazo aliwahidi wananchi nyingi amezitekeleza.
Nao baadhi ya wananchi walimpongeza Mbunge Katambi kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, huku akimuomba awatatulie changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo iliharibiwa na mvua,kufikisha umeme kwenye maeneo ambayo bado, pamoja na umaliziaji wa maboma ya Zahanati yaliyosalia.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk.Elisha Robert akijibu swali la ukamilishaji wa Zahanati kwenye Mkutano wa Mbunge amesema kwanza anamshukuru Rais Samia pamoja na Mbunge Katambi, sababu Manispaa hiyo kuliwa na Maboma 16,lakini 6 yamekamilishwa na yanatoa huduma, huku Zahanati Mbili ya Mwagala na Mwamagunguli zipo hatua za mwisho za ukamilishaji. Mbunge Katambi kesho anaendelea na ziara yake Katika Kata ya Mwamalili na Oldshinyanga.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza na wananchi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza.
Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Saidi Bwanga akizungumza.
Diwani wa Kizumbu Rubeni Kitinya akizungumza.
Viongozi wakiwa Meza Kuu.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Mbunge Katambi.







Wataalamu wakijibu maswali ya wananchi kwenye Mkutano wa Mbunge Katambi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464