WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ARIDHISHWA VIWANGO UPANUZI UWANJA WA NDEGE IBADAKULI-SHINYANGA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ARIDHISHWA VIWANGO UPANUZI UWANJA WA NDEGE IBADAKULI-SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amefanya ziara fupi ya kukagua upanuzi ujenzi wa uwanja wa ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, na kueleza kuridhishwa na viwango vya ujenzi wa uwanja huo, huku akimuagiza Mkandarasi kutoka kampuni ya CHICO,kufunga Taa ili uanze pia kutumika nyakati za usiku.
Majaliwa amebainisha hayo leo Februari 16,2025 katika Uwanja huo wa Ndege Ibadakuli-Shinyanga,wakati alipowasili kwa ajili ya kupaa na ndege akitokea mkoani Simiyu, ambapo jana pia alitua katika uwanja huo,na kupongeza maendeleo ya ujenzi wake.

Amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi mingi ya kimkakati, na kwamba katika upanuzi wa uwanja huo wa Ndege Ibadakuli-Shinyanga, hana wasiwasi na viwango vyake ya ujenzi, kutokana na kwamba Mkandarasi CHICO ametekeleza miradi mingi ya serikali na viwango vyake ni bora.
“Uwanja huu wa Ndege Ibadakuli Hapa Shinyanga umeshakamilika kwa asilimia kubwa, na miundombinu mingi ya muhimu imekamilika, na mimi nimeutumia kwa kutua na kuondoka, ila bado kuna mapungufu ya Taa, hivyo nakuangiza Mkandarasi Chicco weka Taa haraka ili ndege zianze kutua usiku na siyo mchana tu, ili wananchi waanze kupata huduma ikiwamo na mikoa jirani,”amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

“Ndege za ATCL,Serikali, zinasubiri ratiba tu kuanza kuutumia uwanja huu, TANROADS na Msimamizi wa upanuzi ujenzi wa uwanja huu, msimamieni Mkandarasi awekee Taa haraka, ili uwanja uanze kutumika rasmi, na mtumie jengo la zamani la abiria, wakati mkisubiri hili jipya kukamilika,”ameongeza.
Aidha,amesema dhamira ya Serikali ni kurahisha sekta ya usafiri ukiwamo wa Anga, na kwamba karibu mikoa yote hapa nchini vinajengwa viwanja vya Ndege kasoro mikoa ambayo ni mipya.

Ametoa wito pia kwa vijana ambao wamepata ajira kwenye ujenzi wa uwanja huo, kwamba wafanye kazi kwa weledi pamoja na kupata ujuzi, ili mradi huo utakapokamilika kujengwa na wao wafungue makampuni yao ya ujenzi, na kuanza kuchangamkia fursa za ujenzi, sababu wana ujuzi wa kutosha ili miradi hiyo mikubwa ya kimkakati hapo baadae ianze kujengwa na Wazawa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, amempongeza Rais.Dk.Samia Suluhu Hassan,kwamba katika utawala wake ndani ya miaka minne, ameutendea haki mkoa huo ambapo miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa,huku akimuomba Waziri Mkuu kufanya ziara ya kikazi mkoani humo, ombi ambalo lilikubali na kwamba Waziri Mkuu atakwenda kupanga Ratiba.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu, amepongeza Rais Samia kwa kugusa maisha ya wananchi wa Shinyanga, na kwamba uwanja huo wa ndege ulikuwa ni kilio cha muda mrefu, lakini sasa umeshaanza kutumika kwa hatua za awali.
Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samweli Mwambungu, akitoa taarifa ya ujenzi wa uwanja huo wa ndege,amesema barabara ya kutua na kuruka ndege “Runway”imekamilika kwa asilimia 100, uzio 60, Jengo la abiria asilimia 50, na linatarajiwa kukamilika Aprili Mosi mwaka huu.

Amesema kwa upande wa fidia sh.milioni 764 zimeshalipwa kwa wananchi ambao walikuwa jirani na uwanja huo,ili kupisha upanuzi wake, huku zikitolewa pia ajira 160, wazawa wakiwa ni 130, na kwamba Mkandarasi ameshalipwa pesa zake zote, na bado yupo ndani ya mkataba, na gharama za upanuzi wa ujenzi wa uwanja huo ni sh.bilioni 49.

TAZAMA PICHA👇👇
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ziara fupi ya kukagua upanuzi wa ujenzi uwanja wa Ndege-Ibadakuli Shinyanga, wakati alipowasili kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuruka na Ndege akitokea mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkandarasi kutoka Kampuni ya CHICCO nakumpatia maagizo ya kuweka Taa ili Ndege zianze kuruka na kutua nyakati za usiku.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza.
Meneja wa TANROASD Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samweli Mwambungu akitoa taarifa ya upanuzi wa ujenzi wa uwanja wa Ndenge Ibadakuli-Shinyanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua maendeleo ya upanuzi ujenzi uwanja wa Ndege Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, alipo wasili kwenye uwanja wa Ndege Ibadakuli-Shinyanga.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo alipo wasili kwenye uwanja wa Ndege Ibadakuli-Shinyanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amabye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiendelea kusalimiana na viongozi mbalimbali.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaaga viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga, wakati akitaka kuruka na Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli-Shinyanga.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiruka na Ndege katika Uwanja wa Ndege Ibadakuli- Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464