KATAMBI AGUSA MAISHA YA WANANCHI WA IBADAKULI

KATAMBI AGUSA MAISHA YA WANANCHI WA IBADAKULI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu, ameendelea na ziara yake, huku wananchi wa Ibadakuli wakimshukuru kwa kuwatatulia changamoto ambazo zilikuwa kero kubwa.
Wananchi wa Ibadakuli wakizungumza kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mbunge Katambi, uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Rajani, kwa ajili ya kusikiliza kero zao pamoja na kuwaeleza yale ambayo ameyafanya ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge.

Wamesema Kata hiyo ya Ibadakuli, ili kuwa na changamoto nyingi ambazo zilikuwa kero kubwa kwa wananchi ikiwamo ukosefu wa huduma ya umeme, licha ya Kata hiyo kuwa na Kituo kikubwa cha kupoza umeme, lakini wananchi wa maeneo hayo walikuwa gizani.
Wamesema tatizo jingine ilikuwa na ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja likiwamo la Uzogole- Bugwandege, lakini limejengwa na sasa wananchi wanapita bila changamoto zozote.

“Tunamshukuru Katambi amekuwa Mbunge wa kugusa maisha ya wananchi, hapa Ibadakuli tulikuwa na matatizo mengi, Wabunge wengi wamepita lakini walishindwa kuyatatua, lakini wewe kwa muda mfupi umetutatulia,”amesema Shija.
Naye Mbunge Katambi akizungumza na wananchi hao, amesema yeye ni kiongozi ambaye aliwekwa na wananchi wenyewe, hivyo ni lazima awatumikie kuwatatulia matatizo yao, na kwamba kwenye Kata hiyo ya Ibadakuli pia ilikuwa na shida kubwa ya maji,lakini sasa hivi maeneo mengi yana huduma hiyo, na bado miradi inazidi kutekelezwa.

“Hapa Ibadakuli kipindi naingia kwenye Ubunge hapakuwa na huduma ya maji kabisa, madaraja na vivuko havikuwepo,wala umeme, lakini ndani ya miaka yangu minne ya Ubunge vitu vyote hivyo nimetekeleza na tunakwenda kukamilisha kwenye vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na baadhi ya huduma,”amesema Katambi.
Aidha, amesema kwenye Kata hiyo pia kulikuwa na mradi wa kimkakati ambao ujenzi wake ulikuwa unasua sua wa Uwanja wa Ndege,lakini sasa hivi unakwenda kukamilika, huku ndege tayari zikiwa zimeanza kutua nyakati za mchana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alishatua na kuruka kwenye uwanja huo.

Amempongeza pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi kwenye jimbo hilo la Shinyanga Mjini na hata miradi mingi kutekelezwa, sababu kila anapomuomba amekuwa ni mtu wa kutekeleza sababu ya kuguswa na shida za wananchi, na kwamba katika uchaguzi Mkuu 2025 atashinda kwa kishindo kutokana na kukubalika na wananchi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu,akizungumza wananchi wa Ibadakuli kwenye Mkutano wa Hadhara.

Wananchi wa Ibadakuli wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mbunge Katambi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464