Dodoma jiji FC yapata ajali basi lapinduka mara mbili
![](https://www.ippmedia.com/storage/post-feature-images/01JKQKX4FCFVJ99A2GFB5F08WY.webp)
Picha:Mtandao
Dodoma jiji FC yapata ajali basi lapinduka mara mbili.
Basi la timu ya Dodoma Jiji FC limepata ajali ya asubuhi ya leo maeneo ya Nangurukuru kuelekea Somanga mkoani Lindi likitokea mjini Ruangwa ambako jana walicheza mechi ya ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo FC.
Inaelezwa kuwa basi hilo lilipinduka mara mbili. Taarifa zinadai wachezaji wengi wamepata majeraha na hakuna kifo kilicho ripotiwa
Katibu Mkuu wa Timu hiyo, fortunatus Johnson amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba kwa sasa huduma ya uokozi inaendelea.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464