RC MACHA AWATAKA WANUFAIKA WA MIKOPO ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI WAIREJESHE KWA WAKATI

WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

Na. Paul Kasembo, KISHAPU DC.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kuwanufaisha na wengine pia.
RC Shinyanga Anamringi Macha.

Hayo yamesemwa leo tarehe 13 Februari, 2025 wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa Hundi kwa vikundi nufaika yenye zaidi ya Milioni 587.5 hafla iliyofanyika katika viwanja vya Halmashaui ya Wilaya ya Kishapu nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Victor Masindi, viongozi wa vyama vya siasa, wataalam wakionhozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed pamoja na wananchi.
DC Kishapu Victor Masindi.

"Pamoja na kuwapongeza kwa hatua hii, niwatake sasa kuhakikisha mnarejesha mikopo hii mnayokopeshwa kwa wakati ili Serikali iweze kuwapatia na vikundi vingine na mwisho tuweze kufikia lengo kusudiwa kwa Serikali na wananchi kwa ujumla wake," amesema RC Macha.

Hii inafuatia Kamati ya Huduma za Mikopo ngazi ya Halmashauri kufanya uhakiki wa nyaraka za vikundi hivyo vilivyowasilisha maombi na kisha ziara ya ukaguzi wa miradi ilifanyika ili kuona uhalisia na baadae vikao vya tathimini vya kamati vilifanyika kwa pamoja na timu ya Menejimenti ambapo ilijiridhisha pasipokuwa na shaka kisha kuridhia kutolewa kwa mikopo hiyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imetenga takribani Milioni 726. 8 kwa ajili ga kukopesha vikundi ambapo dirisha la maombi ya mikopo lilipokea kwa vikundi 162 huku vya wanawake ni 102, vijana 54 na watu wenye ulemavu 6 na kwamba vikundi 59 kwa awamu ya kwanza ambapo vikundi 35 ni vya wanawake,vijana vikundi 22 na watu wenye ulemavu 2 huku akiwasisitiza kwenda kuitendea haki na kuweza kufikia lengo kusudiwa la Serikali.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464