RC MACHA ASISITIZA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA BARABARA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, amesisitiza suala la utunzaji wa miundombinu ya barabara,ili idumu kwa muda mrefu kuwa hudumia wananchi.
Amebainisha hayo leo Februari 26,2025 wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara.
Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,imefanyakazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara,lakini katika Mkoa wa Shinyanga kuna tatizo la kutozitunza barabara hizo.
“Katika Mkoa wa Shinyanga tusipomshukuru Rais Samia juu ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja,tutakuwa wachoyo wa fadhira,lakini tunakabiliwa na changamoto ya utunzaji wa barabara,”amesema Macha.
“Barabara zetu ukiangalia mitaro imejaa takataka, imeota majani, chupa za maji zimetupwa umo,na mvua zikinyesha maji yanakosa pakupita na kusababisha kingo kuanza kubomoka,”ameongeza.
Ametolea pia mfano wa barabara ya Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama,kwamba barabara hiyo ni mpya lakini mitaro yake imaanza kujaa uchafu.
Ameonya pia tabia ya baadhi ya watu kwa waache kuchimba mchanga kando ya hifadhi ya barabara, na kuigusia barabara ya Nyamilangano iliyopo Ushetu, kwamba tayari mashimo yameanza kumega barabara.
“TARURA,TANROADS na Wakurugenzi wa Halmashauri acheni kuandikiana barua kwenye suala la utunzaji wa barabara,itaneni mkae kwenye vikao na kujadili kwa pamoja juu ya utunzaji wa barabara hizi, sababu kila mmoja ukimuuliza mnasukumiana nilishamwandikia barua flani, hiyo sitaki kaeni vikao,”amesema Macha.
Ametahadharisha pia watu ambao wanapewa Vitalu vya kuotesha miche kando ya hifadhi ya barabara, au kufanya shughuli zingine, kwamba wapewe mikataba pamoja na uangalizi mkubwa, ili wasije kujenga makazi ya kudumu na hata kupelekewa huduma za kijaamii, yakiwamo maji na umeme, na mwisho wasiku wanakataa kuondoka kuwa maeneo hayo ni ya kwao.
Amegiza pia uwepo na usimamizi mzuri kwa Wakandarasi ambao wanajenga barabara hasa wakati wa kumaliza kazi zao,kuwa wazimalize kwa ufanisi na siyo kulipua, sababu kuna baadhi ya barabara amekuwa akishuhudia “finishing” yake kuwa mbovu.
Pia, amegusia suala la Wakandarsi kuweka vifusi kwenye barabara na kisha kutokomea kwa muda mrefu, kwamba tatizo hilo nalo liangaliwe ili kutozuia shughuli za kiuchumi kutofanyika kwa wananchi sababu ya vifusi hivyo.
Amesisitiza pia suala la mikataba na Wakandarasi liangaliwe pale wanapokwenda kuchimba mashimo kwenye maeneo ya watu, kuwa wakimaliza shughuli zao waone namna ya kuyafukia, au kuweka mazingira mazuri mashimo hayo yatumike kwenyeshea maji mifugo,kufugia samaki,na siyo kuachwa hovyo na hata kusababisha maafa.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akifungua kikao cha Bodi ya Barabara.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464