Mbunge Patrobas Katambi.
KATAMBI ATOA MSAADA WA KITIMWENDO KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, ametoa msaada wa Kitimwendo kwa mtoto mwenye ulemavu Anjel Daniel (6)mkazi wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Msaada huo umetolewa leo Februari 16,2025 na Katibu wa Mbunge Samweli Jackson,kwa niaba ya Mbunge Katambi.
Samweli akizungumza wakati wa kukabidhi Kitimwendo, amesema Mbunge Katambi amekuwa akiguswa sana na watu wenye uhitaji mbalimbali, na amekuwa akitatua changamoto zao mara kwa mara, na kwamba baada ya kupata maombi juu mtoto huyo kuhitaji Kitimwendo,aliguswa na leo amekikabidhi rasmi kwa mama yake mzazi.
“Kwaniaba ya Mbunge Katambi namkabidhi Mama mzazi wa mtoto huyu Kitimwendo,na ameahidi kuendelea kumsaidia zaidi,na ameomba watu wote wenye watoto walio na ulemavu na wanahitaji kusaidiwa wasiwafiche ndani,ikiwa yeye yupo kwa ajili yao na ndiyo Wizara ambayo anaifanyia kazi,”amesema Samweli.
Mama mzazi wa mtoto huyo Doricas Daudi Yacob, amemshukuru Mbunge Katambi kwa msaada wake huo mkubwa,na amemuomba aendelee na moyo huo huo wa kusaidia watu wenye uhitaji,ikiwa amekuwa akimuona kwenye vyombo vya habari akisaidia watu wengi.
Mdau wa maendeleo Hashimu Issa,amesema walimuona Mama wa Mtoto huyo akiomba msaada kupitia kwenye vyombo vya habari, ndipo wakaguswa na kuamua kumsaidia pia dawa za matibabu ya mtoto wake,huku akimtafuta Mbunge Katambi na kumuomba amsaidie,na sasa ameanza kutekeleza kwa vitendo,na kumpogeza namna anavyoguswa na watu wenye uhitaji.
TAZAMA PICHA👇👇
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464