KATAMBI ASIMIKWA NA WAZEE OLDSHINYANGA KUWA MTAWALA,APEWA JINA LA CHIFU GUDILILWA "NDELEJI" KUTOKANA UTENDAJI WAKE KAZI NA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI


KATAMBI ASIMIKWA NA WAZEE OLDSHINYANGA KUWA MTAWALA, APEWA JINA LA CHIFU GUDILILWA "NDELEJI" KUTOKANA UTENDAJI WAKE KAZI NA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

BARAZA la ushauri la wazee Kata ya Oldshinyanga,wamemsimika Mbunge Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Watu wenye ulemavu kuwa Mtawala,na kupewa jina la Chifu Gudiliwa yani "Ndeleji" likiwa na maana ya mfuatiliaji na mtatuzi wa changamoto za wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Usimikwaji huo umefanyika leo Februari 24,2025,ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Kata ya Oldshinyanga Stephano Tanu.

Tanu akizungumza kabla ya Mbunge Katambi kusimikwa na Mzee Idd Pyalimi, amesema wazee wameridhishwa na kazi kubwa ambayo anaifanya Mbunge huyo,na kwamba Shinyanga haijawahi kuwa na Mbunge ambaye anaguswa na matatizo ya wananchi na kutatua kero zao.
"Katambi ametuheshimisha sana, hivyo sisi wazee tunamsimika na kumpatia taji la Utawala, ili aendelee kuwa kiongozi wetu tena na kutuletea maendeleo zaidi, sababu shinyanga ya sasa siyo ile ya zamani imepiga hatua kubwa kimaendeleo," amesema Tanu.

Naye Mzee Iddi Pyalimi,mara baada ya kumaliza kumsimika Mbunge Katambi, walimpatia jina la chifu Gudiliwa "Ndeleji", ili aendelee kufuatilia masuala ya maendeleo na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Mbunge Katambi,ameashukuru wazee hao kwa kumsimika pamoja na kumpatia jina la Chief Gudililwa "Ndeleji" na kwamba jina hilo amelipokea, huku akihidi kuendelea kuchapa kazi zaidi na kuwaletea maendeleo.

"Wazee wangu mmeniheshimisha sana na kunipatia nguvu ya kufanya kazi usiku na mchana,ili niwatumikie wananchi wa Shinyanga na kuwaletea maendeleo zaidi," amesema Katambi.

Amesema ndani ya miaka Minne ya Ubunge wake ametekeleza ahadi nyingi ambazo aliahidi wananchi katika sekta mbalimbali ikiwamo ya Elimu,Afya,Maji,Umeme,na miundombinu ya barabara.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akisimikwa na wazee wa Oldshinyanga kuwa Mtawala na kupewa jina la Gudililwa yani Ndeleji lenye maana ya mfuatiliaji wa mambo na mtatuzi wa changamoto za wananchi.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza na wananchi wa Oldshinyanga.
Diwani wa Oldshinyanga Enock Lyeta akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Anord Makombe akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464