.jpg)
Na Mwandishi wetu.
AFISA Elimu wa kata ya Masengwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Shabani Nzila ameongoza zoezi la upandaji wa miti katika shule tano za msingi na Sekondari.
Zoezi hilo
liliendeshwa tarehe 18/02/2025 na Afisa huyo katika mida tofauti tofauti baada ya kutoa
miti na kuhamasisha wanafunzi wa shule hizo kushirikiana na walimu katika
kuipanda.
Afisa Elimu Mwalimu Nzila
amezitaja shule hizo kuwa ni
Bubale,Ikonda, Masengwa shule ya msingi na Sekondari ,Ilobashi .
“Walimu ambao hawakuwa na vipindi kwa siku hiyo na wanafunzi tumeshirikiana vizuri tumeweza kupanda na kila mtu alikuwa akipanda miti miwili”amesema Mwalimu Nzila.
Mwalimu Nzila amesema wamepanda miti hiyo pia katika ofisi ya mtendaji wa kata kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464