MRINDOKO : CCM NI IMARA, TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, amewaomba Watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusema kuwa CCM ni chama imara kinachopaswa kuendelea kushika dola. 

Katika ziara yake ziara yake na wajumbe wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini, katika kata ya Kitangili, iliyofanyika leo Februari 19,2025 , Mrindoko ameonyesha mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu, akisisitiza kwamba CCM inajivunia mafanikio katika sekta mbalimbali.

Mrindoko amesema CCM imeendelea kuwa imara na itaendelea kushika dola, akisema: "Chama chetu kimempitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kugombea Urais mwaka 2025 pamoja na Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza. CCM ipo imara, tumejipanga vizuri, wanaopita pita tutawachapa kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2025" .

Amewataka wanachama na Watanzania kwa ujumla kusimama imara kumuunga mkono Rais Samia na mgombea mwenza.

Pia, ametoa wito kwa wazazi kuchangia fedha kwa ajili ya chakula cha wanafunzi shuleni, akisema ni muhimu kuhakikisha watoto wanapata chakula cha kutosha ili wasikose masomo kwa njaa.

Mjumbe mwingine wa kamati ya utekelezaji wilaya ya Shinyanga Mjini, Giti Boniphace, ametoa wito kwa jamii kuwalea watoto kwa njia bora. 

Giti Boniphace

Giti amehimiza wazazi kuwapeleka watoto shuleni, kanisani, na msikitini, na kuwatunza kwa heshima, ili wawe na elimu ya kidunia na ile ya dini. 

Vilevile, amehamasisha kuhusu umuhimu wa kuwafundisha watoto kazi za mikono.

"Tuwasaidie watoto wajue kazi za mikono, sasa hivi tunapata wakamwana hawajui hata kupika. Akina mama tukaze, wazazi tuwalee watoto, tuwajibike”,amesema Giti.

Ziara ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini inaendelea kutembelea kata zote za Jimbo la Shinyanga Mjini kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464