NAIBU WAZIRI HAMIS MWINJUMA AFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI,ASISITIZA UTOAJI TAARIFA SAHIHI ZA UCHAGUZI MKUU 2025


Waandishi wa habari wasisitizwa kutoa taarifa sahihi za uchaguzi mkuu 2025

Na Marco Maduhu,DODOMA

NAIBU Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma, amewasisitiza waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi za uchaguzi Mkuu 2025,wa kuchagua Madiwani,Wabunge na Rais.
Amebainisha hayo leo Februari 14,2025 wakati akifunga mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini, Jijijini Dodoma, ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambao umedumu kwa muda wa siku mbili.

Amesema kupitia mafunzo hayo anaamini waandishi wamejifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma, na kwamba yamewajenga hasa kwenye utoaji wa taarifa sahihi hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
"vyombo vya habari ni muhimu sana kuelekea kwenye uchaguzi kuu wa mwaka huu, na msipotoa taarifa sahihi mnaweza kuchangia demokrasia kuzama,"amesema Mwinjuma.

"Hivyo nawasihi mtoe taarifa sahihi, zisizoegemea upande wowote, na mhabarishe umma ili wafanye machaguo sahihi kwa kuchagua viongozi wanaowataka,"ameongeza.
Amesisitiza pia suala la matumizi ya lugha sahihi ya kiswahili katika utangazaji, ili kuilinda lugha hiyo na kutokubali kuharibiwa, bali waitumie kwa ufasaha.

Aidha,amesema serikali ipo pamoja na sekta ya habari,na kwamba milango ya Wizara ipo wazi, na kusisitiza dhamira ya Rais Samia suluhu Hassani ni kuikuza Sekta hiyo,na ndiyo maana alipoingia Madarakani alivifungilia vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vimefungiwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka, naye amesisitiza waandishi wa habari wawe makini wanapo ripoti habari za uchaguzi na kutoongeza "Chumvi", pamoja na kutoa uwiano sawa wa muda wa vipindi kwa wagombea.

Amesema mikutano hiyo wameianzisha TCRA,kwa malengo ya kukuza sekta ya utangazaji.
Kauli mbiu ya Mkutano huo inasema "wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

TAZAMA PICHA👇👇
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464