
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akikagua pamba katika kijiji cha Mwamanota kata ya Ngofila wilayani Kishapu
Suzy Butondo, Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amekemea tabia ya baadhi ya vijana kukaa mjini bila kazi kwa madai ya kutokuwa na ajila badala yake amewataka wachangamkie fulsa ya kilimo hasa Vijijini kitendo kitakachowainua kiuchumi na kuepuka utegemezi.
Hayo ameyasema leo February 18,2025 wakati akikagua maendeleo ya kilimo cha zao la pamba katika Kata ya Ngofila Wilayani Kishapu Mkoani humo, ambapo amekagua mashamba mbalimbali katoka kata hiyo likiwemo shamba la Ester Mwandu wa kijiji cha Mwamanota katika kata hiyo.
Macha wakati akikagua mashamba hayo amekutana na Maafisa ugani wakiendelea kuwaelimisha wakulima wa zao la pamba, ambalo limeanza kuleta matokeo chanya kwa familia na Jamii kwa ujumla, ambapo aliwashauri waendelee kuwaelekeza wakulima ili waondokane na kilimo cha kizamani
Macha amesema vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mjini na kuacha kujikita kwenye kilimo cha zao la pamba, ambacho kinaweza kuwainua kiuchumi,na kuondokana na umasikini.
‘’Inasikitisha sana kuona baadhi ya vijana wa Mkoa wa Shinyanga ambao wamekaa makundi pale Mjini wakidai kuwa hakuna ajila inawezekanaje Serikali ikaajili mtu kutoka Arusha ikamleta Kishapu na ikaacha kijana wa Mkoa wake ,huu ni uvivu, hivyo niwaombe wachangamkie fulsa ya kilimo hasa huku kijijini fulsa zipo.’’ amesema Macha.
‘Nawaona maafisa kilimo wametoka mikoa ya mbali wamekuja kwa ajili ya kujitolea wanawasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija, kuna baadhi yawakulima wamelima heka moja kwa kitaalamu na wamepata kilo 800 mwingine kalima heka nne kapata kilo 4400, lakini wanaolima kiholela hawapati kilo hizo wanaishia kilo kidogo tu’.amesema Macha
Aidha amewashukuru wote waliolima zao la pamba, kwani ndiyo kilimo cha zao la biashara kinachoweza kubadili maisha ya vijana, hivyo amewataka wajitahidi kulima zao hilo, kwani kuna fulsa za kukopeshwa fedha na kuweza kuendeleza zao hilo kwa ufasaha zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Peter Niclous Masindi amewataka Maafisa Ugani kutafuta maeneo kwaajili ya kilimo ili kuwa shamba darasa kwa wengine na kujiongezea kipato.
Aidha afisa kilimo kutoka wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula amesema maafisa kilimo wamesambazwa kila kila kata na kila kijiji wanafanya kazi na wanawapa elimu wakulima kulima kilimo chenye tija, hivyo jamii inaendelea kubadilika na kuachana na kilimo cha kizamani.
Nao baadhi ya wakulima wa zao hilo akiwemo Esta Mwandu mkazi wa Kijiji cha Mwamanota Kata ya Ngofila wamesema kupitia mchango wa elimu ya kilimo bora kutoka kwa Maafisa Ugani wa eneo hilo wamefanikiwa kupata mazao mengi yenye ubora wa hali ya juu.
Tunawashukuru sana hawa maafisa kilimo mliotuletea wanatuelekeza vizuri ndiyo maana mnaona mashamba yenye afya kama haya yanazidi kupendeza tu, sasa hivi nimelima heka moja lakini mwakani nitaongeza heka ziwe hata mbili ili niweze kuongeza kipato changu’.
Aidha wananchi hao walitoa kilio chao kwa mkuu wa mkoa kwamba hawana maji safi na salama katika kata hiyo,maji ambayo wanatumia si salama ambayo nayo wanafuata zaidi ya kilomita 10 hali ambayo imekuwa ikisababisha watoto wa kike kupata ujauzito kabla hawajamaliza masomo yao ya kidato cha nne.
‘ Sisi kilio chetu kikubwa hapa Ngofila ni maji hatuna maji safi na salama na maji tunayotumia si salama sana ambayo tunayafuata kilomita zaidi ya 10, na tunaamka saa 10 ya usiku kufuata maji na hali hii imesababisha wanafunzi wa kike wengi kupata mimba na kushindwa kuendelea na masomo yao tunaiomba serikali ituletee maji ili kuponya ndoa zetu hazina amani kabisa’amesema Agnes Butondo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza kwenye ziara ya mkuu wa mkoa


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akizungumza na wananchi wa kata ya Ngofila wilayani Kishapu

Afisa kilimo wa wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula akifafanua jambo kwa mkuu wa mkoa juu ya kilimo cha zao la pamba
Wananchi wa kata ya Ngofila wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akizungumza
Sungu sungu wa kata ya Ngofila wakiingia uwanjani kumpokea mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akionyesha zawadi ya tikiti alilopewa na wakulima wa kata ya Ngofila
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na mkuu wa wilaya ya Kishapu wakipokea zawadi ya tikiti kutoka kwa wanawake wa Ngofila
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha akionyesha zawadi ya tikiti alilopewa na wakulima wa kata ya Ngofila
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464