UTAMBUZI WA MIFUGO SASA NI BURE - DKT. KIJAJI

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati wa mkutano baina yake na Wafugaji uliofanyika Februari 19, 2025 jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti.
◼️Aeleza namna Serikali ilivyoshughulikia changamoto zote zilizolalamikiwa awali

◼️Apiga marufuku ukamatwaji wa mifugo ambayo haijatambuliwa

***

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa zoezi la Utambuzi wa wanyama sasa litafanyika bila gharama yoyote kutoka kwa wafugaji baada ya Serikali kuamua kugharamia zoezi hilo.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo wakati wa mkutano baina yake na wafugaji uliofanyika Februari 19, 2025 jijini Dodoma ambao ulilenga kuwahamasisha kuekelea kwenye kampeni yaa kitaifa ya chanjo naa Utambuzi wa Mifugo.

“Mhe. Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kufanya tathmini ya zoezi hili na kufanyia kazi changamoto zote zilizolalamikiwa hapo awali ambapo mojawapo ilikuwa ni bei kubwa uwekaji hereni kwa mfugo na ndio maana Serikali sasa imeamua lifanyike bila gharama yoyote”, amesema Mhe. Dkt. Kijaji.

Aidha Mhe. Dkt. Kijaji amezuia ukamatwaji wa mifugo ambayo haitakuwa imefanyiwa utambuzi ambapo amewataka watalaam wa sekta ya Mifugo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo huku akitoa rai kwa wafugaji kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kutambua mifugo yao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464