UWT KATA YA MJINI WAADHIMISHA MIAKA 48 YA CCM KWA KUTOA ZAWADI KWA SHULE ZA MSINGI MWENGE NA TOWN



Suzy Butondo, Shinyanga

Umoja wa wanawake Tanzania UWT Kata ya Shinyanga Mjini katika kuadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM wametoa zawadi ya sabuni za kusafishia vyoo pamoja na mifagio kwa ajili ya kufanyia usafi katika Shule za Msingi Mwenge na Town .

Akikabidhi zawadi hizo Mwenyekiti wa UWT Kata ya Mjini Mwiza Said amesema wametoa zawadi hizo wametoa ni kwa ajili ya kufanya usafi na kujikinga na magonjwa ya maambukizi.


"Sisi Baraza la UWT Kata ya Mjini tumeona kuadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM tulete sabuni hizi na mifagio kwa watoto wetu ili kuendeleza usafi kwa watoto wetu, wasipatwe na magonjwa ya maambukizi"amesema Mwenyekiti Mwiza.


Katibu wa UWT Kata ya Mjini Khadija Kasimu Amesema wameona watoe sabuni na mifagio ili kuweza kudumisha usafi kwa watoto, na kuadhimisha kuzaliwa kwa miaka 48 ya CCM.

Aidha diwani viti maalumu Moshi kanji ambaye ni mlezi wa Kata hiyo amesema wanawake wa UWT Mjini wameleta hicho kidogo na kuwaomba wapokee kitasaidia kufanyia usafi.

Walimu wakuu wa Shule hizo wameshukuru kupatiwa sabuni hizo na mifagio na kuwaomba wadau wengine waendelee kuwakumbuka kwani bado Wana mahitaji mbalimbali































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464