Wanawake wa UWT kata ya Ndembezi wakikabidhi akiwemo katibu muenezi wa chama cha mapinduzi kata ya Ndembezi Issa Sitima wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kukabidhi zawadi zao katika kituo cha Shinyanga Society Orphans
Suzy Butondo, Shinyanga
Umoja wa Wanawake Tanzania UWT kata ya Ndembezi ukiongozwa na mwenyekiti wake Lina Kazimily umeadhimisha kuzaliwa kwa miaka 48 ya CCM kwa kutoa zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Shinyanga Society Orphans kilichopo maeneo ya Bushushu katika manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT kata ya Ndembezi na viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakikabidhi msaada huo, amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuwakumbuka watoto hao, kwani wanajisikia vizuri wakiona wadau mbalimbali wakiwapa zawadi misaada mbalimbali.
“Tumeamua kufanya maadhimisho yetu ya kuzaliwa kwa miaka 48 ya CCM kwa kuwatembelea watoto, hawa hivyo tumeona tuje na zawadi kidogo tunaomba mpokee tutaendelea kuja mara kwa mara kuwaona"amesema Lina.
Mkurugenzi wa kituo hicho Ayam Ally Said ameushukuru umoja huo kwa kutoa zawadi hizo “tunawashukuru sana kwa kuwakumbuka watoto wetu hawa tunawaombea kwa Mungu awabariki pale mlipotoa muongezewe mara dufu”.
Wanawake wa UWT akiwemo katibu muenezi wa kata ya Ndembezi wakikabidhi zawadi zao katika kituo cha Shinyanga Society Orphans