WABUNGE WAPONGEZA MIGODI YA BARRICK-TWIGA KWA UTUNZAJI MAZINGIRA, UTEKELEZAJI WA MAUDHUI YA NDANI

 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika sehemu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati wa ziara hiyo
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick -Twiga Bulyanhulu, Victor Lule akizungumza. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa  akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Kilumbe Ng’enda
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika sehemu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika sehemu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu

***

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Migodi wa Barrick naTwiga kwa kuendelea kufuata viwango vya kimataifa na vinavyokubalika vya uchimbaji wa madini vinavyoimarisha utunzaji wa mazingira, usalama mahala pa kazi kwa maslahi mapana ya wafanyakazi na wananchi wanaozunguka mgodi.

Akizungumza kwenye ziara ya siku ya pili ya kamati hiyo mwishoni mwa wiki migodi ya Barrick Twiga ya Bulyanhulu na Buzwagi ambao upo kwenye hatua za mwisho za ufungaji na kuwa kongani maalumu , Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kilumbe Ng’enda alisema kwamba migodi ya Barrick yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga iko mstari wa mbele katika kuwasaidia watanzania kupitia kanuni ya maudhui ya ndani (Local Content) na Uwajibikaji wa Jamii (CSR).

“Hii ni mara ya pili tunazuru Mgodi wa Barrick Twiga kuona maendeleo ya uchimbaji na upanuzi wa shughuli hizo za hasa utafiti, usindikaji na shughuli zingine za kila siku ambazo zina matokeo Chanya kwa jamii inayozunguka mgodi husika,” alibainisha.

Alisisitiza kwamba Mgodi wa Barrick -Twiga umetilia mkazo sekta zote muhimu zinazohitajika kwa matumizi ya binadamu kama vile elimu, uchimbaji wa visima maji, vituo vya afya, na programu mbalimbali zinazolenga kusaidia wananchi wa eneo linalozunguka mgodi.

“Tumeambiwa na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu kwamba muda wa maisha ya mgodi wa Bulyanhulu ni miaka 25 ijayo, hivyo bado Bunge, Serikali na mgodi wenyewe tunapaswa kuendelea kushirikiana kwa karibu kuhakikisha faida za uwepo wa mgodi zinasambaa kwa wananchi wa kawaida na nchini kwa ujumla pamoja wakati wa kipindi chote hiki,” alibainisha.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa amewataka makampuni mengine ya madini nchini kuiga mwenendo wa mgodi wa Barrick-Twiga katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika sekta ya uchimbaji madini.

Alisema kuwa serikali kupitia wizara ya madini imeona mafanikio makubwa katika utekelezaji wa kanuni za maudhui ya ndani (Local content) na uwajibikaji wa jamii (CSR) ambazo zinakusudia kuwaondoa watanzania wa kawaida katika umaskini.

Alibainisha kuwa lengo la serikali kuanzisha kanuni hizi mbili ni kuhamasisha ushirikishwaji na kukuza uhusiano wa kijamii kati ya mgodi na wananchi wa eneo hilo lakini pia kuona Watanzania wakishiriki katika uwekezaji wa biashara ya madini nchini.

Naibu Waziri alieleza zaidi kufuata na kufanya kwa ufanisi maudhui ya ndani na uwajibikaji kwa jamii na kufungua milango kwa watanzania kushiriki katika biashara ya uchimbaji madini ni mafanikio yanayoleta ustawi wa jamii.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick -Twiga Bulyanhulu, Victor Lule alisema kampuni inashukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ziara rasmi kwenye mgodi huo ambayo inawawezesha kuelewa shughuli za mgodi na utendaji kazi wake wa kila siku kuanzia utafiti , uchakataji na taratibu zingine ndani ya mgodi.


Alisema mgodi unatekeleza kikamilifu kanuni za uwajibikaji wa jamii (CSR) na sheria za CSR na maudhui ya ndani kwani unalenga hasa kuhamasisha na kujenga uwezo wa Watanzania.


“Tunaendelea kuwafundisha na kuwajengea uwezo wafanyakazi wetu kuhusu matumizi ya mashine za kisasa za uchimbaji madini, teknolojia na ujuzi wa kiufundi ili kuhakikisha kuwa tuna rasiliamali watu wenye uelewa wa kutosha wa teknolojia kwa sababu pia tuna watalaamu wachache kutoka nje na ni muhimu ujuzi wao unabaki hapa nyumbani ,” alibainisha.

“Hadi sasa, tuna asilimia 11 ya wanawake katika nafasi mbalimbali hapa Bulyanhulu, tunatekeleza tunachosema tunapohamasisha wanawake katika sekta ya uchimbaji madini hapa nchini,” alieleza.


Alisisitiza kuwa kampuni ya hiyo ya uchimbaji madini itaendelea kuelimisha wajasiriamali na wasambazaji wa ndani jinsi ya kufanya biashara na makampuni ya madini, jinsi ya kusajili makampuni yao na kushiriki katika warsha za mafunzo, semina na mikutano ili kujenga uhusiano wa kudumu na wenye manufaa kwa nchini nzima.

Bwana Lule alieleza kuwa kampuni ya madini ina asilimia 96 ya wafanyakazi wake ambao ni Watanzania, baadhi yao wakiwa kwenye ngazi za usimamizi, jambo linalothibitisha wazi kuwa Barrick -Twiga inakuza dhana ya maudhui ya ndani.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika sehemu ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati wa ziara hiyo
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464