WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI WAPONGEZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IGALUKILO

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko wakitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini imeeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo, Februari 19, 2025, wakati wa ziara yake na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Wilaya ya Shinyanga Mjini, katika kata ya Kizumbi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, amesema ujenzi wa shule hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuboresha sekta ya elimu.

"Tumetembelea mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kitongoji cha Igalukilo, Kata ya Kizumbi. Shule hii ni nzuri, inajengwa kwa ubora wa hali ya juu. Tumeshuhudia madarasa manne yakiwa tayari kutumika, ofisi ya walimu iko tayari. Tunatarajia shule hii itaanza kutumika hivi karibuni," amesema Mrindoko.

Fue Mrindoko

Ameongeza kusema, "Ninawapongeza sana kwa ushirikiano wenu mzuri, mmesimamia vyema ujenzi huu. Ninakupongeza Mheshimiwa Diwani, wazazi na walimu kwa usimamizi bora wa ujenzi wa shule hii.. Hakika hii inaonesha kwa namna gani Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha sekta ya elimu".

Pia, Mrindoko ametoa wito kwa wazazi kuchangia fedha kwa ajili ya chakula cha wanafunzi shuleni, akisema: "Niwaombe wazazi tushirikiane kutoa fedha za chakula ili kuhakikisha watoto wetu hawaishi kwa shida."

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kizumbi, Reuben Kitinya, ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 603 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya, akisema itasaidia kupunguza umbali wa takribani kilomita 8 ambao wanafunzi walikuwa wakitembea hadi kufika Shule ya Sekondari Kizumbi.

Reuben Kitinya

"Maendeleo ya ujenzi ni mazuri. Madarasa mapya yapo tayari kutumika, maabara tatu zinajengwa, pamoja na maktaba na jengo la kompyuta. Tunatarajia ifikapo Aprili, 2025, ujenzi utakuwa umekamilika. Hata hivyo, tunataka ujenzi wa vyoo ukamilike ili masomo yaendelee kwa wanafunzi 102," alisema Kitinya.

Amefafanua zaidi kwamba, "Mwezi Machi, 2025, wanafunzi 102 wanatarajia watahamia na kuanza masomo katika shule hii ya Sekondari Igalukilo, ambayo itapokea wanafunzi kutoka shule tatu za msingi: Mwamashele, Lyandu, na Bugayambele."

Diwani Kitinya ameongeza kuwa, mbali na maendeleo ya sekta ya elimu, Kata ya Kizumbi miradi ya umeme inazidi kusonga mbele, huku huduma za maji zikipanuliwa karibu na kila kitongoji.

Mwalimu Msimamizi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Igalukilo, Maliki Yazidi Nofel, amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulianza rasmi Septemba 1, 2024, na ulitarajiwa kukamilika Desemba 30, 2024, lakini ulikwama kidogo kutokana na changamoto za mkandarasi. 

Amesema kuwa Serikali ilitoa kiasi cha shilingi 603,890,563/- kwa ajili ya shule hiyo.

Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wanaendelea na ziara yao ya kutembelea kata zote za Jimbo la Shinyanga Mjini, ambapo lengo kuu ni kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM, kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuangalia hali ya uhai wa chama, na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko  (katikati) akiwa katika moja ya vyoo vya wanafunzi vinavyojengwa katika shule mpya ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko wakitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko wakitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Igalukilo, iliyopo katika Kata ya Kizumbi, Manispaa ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464