KATAMBI ASHIRIKI NA WANANCHI UJENZI WA MSINGI ZAHANATI YA IBINZAMATA,ACHANGIA MILIONI 10

KATAMBI ASHIRIKI NA WANANCHI UJENZI WA MSINGI ZAHANATI YA IBINZAMATA,ACHANGIA MILIONI 10

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu,ameshiriki na wananchi ujenzi wa msingi wa Zahanati ya Ibanzamata,pamoja na kuchangia sh.milioni 10.
Ameshiriki ujenzi wa msingi huo leo Marchi 1,2025 akiwa amembatana na viongozi mbalimbali wa chama,wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe.

Amewapongeza wananchi wa Ibinzamata kwa kujitoa katika masuala ya maendeleo,hivyo ameamua kushirikiana nao kwenye ujenzi wa Zahanati hiyo,na kwamba atahakikisha inakamilika na kuanza kutoa huduma.
"ninefurahishwa na nyie wananchi kwa kujitoa katika masuala ya maendeleo juu ya ujenzi wa Zahanati hii, na mimi nitachangia sh.milioni 10 na tutashirikiana hadi kufikia hatua ya Renta,na baada ya hapo tutatafuta fedha ili kuikamilisha kabisa,"amesema Katambi.


Aidha,amesema ndani ya miaka yake Minne ya Ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini kwa upande wa sekta ya Afya, ameshajenga Zahanati mpya 6 na mbili zipo katika hatua ya mwisho ya ukamilishaji ikiwamo ya Mwagala na Mwamagunguli ambapo zitafika Zahanati 8.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe,amempongeza Mbunge Katambi kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo,na kuwashukuru wananchi wa Ibinzamata kwa kujitoa katika mambo ya maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi wa Ibinzamata akiwamo Mabagwe Ibrahimu na Fatuma Bundala,kwa nyakati tofauti wamesema wamewiwa kuanza ujenzi wa Zahanati kwenye Kata hiyo sababu ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Wamemshukuru Mbunge Katambi kwa kuwaunga mkono katika ujenzi wa Zahanati ambayo kwa sasa ipo hatua ya msingi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464