UPEPO WA KATAMBI WANG’OA KIGOGO WA CHADEMA


Katambi akimpokea Kada wa Chadema Jacob Saulo aliyehamia CCM.

UPEPO WA KATAMBI WANG’OA KIGOGO WA CHADEMA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ameendelea na ziara yake ya Kata kwa Kata,ambapo akiwa Kitangili akielezea yale ambayo ameyatekeleza kwa kipindi cha miaka yake Minne ya Ubunge,Kada wa CHADEMA Jacob Saulo ameamua kukihama Chama hicho na kuhamia CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe(kulia)akimpokea Kada wa Chadema Jacob Saulo.

Mkutano huo wa Katambi umefanyika leo March 1,2025 katika shule ya Msingi Kitangili, na kuhudhuliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Kitangili, pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama wilaya ya Shinyanga Mjini.

Kanda huyo wa Jacob Saulo, ambaye pia alikuwa Mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Songambele Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga kwa Tiketi ya CHADEMA, amesema kwamba, ameamua kujiunga na CCM baada ya kuguswa na maendeleo ambayo ameyafanya Mbunge Katambi.
“nimeamua kurudi nyumbani CCM,naombeni mnipokee na mnisamehe, nimeona mambo makubwa ambayo ameyafanya Mbunge Katambi ya kimaendeleo sina sababu ya kuendelea kubaki Chadema,”amesema Jacob.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, amesema amefurahishwa na Kanda huyo wa Chadema kurudi CCM na kumkaribisha kwenye Chama ambacho kipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe, amempokea Kada huyo kwa Chadema na kusema kwamba taratibu zingine zitafuata za kumsajili ili awe Mwanachama Rasmi wa CCM
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464