NAIBU WAZIRI KATAMBI AHUDHURIA MSIBA WA MWANAMKE MWENYE UALBINO ALIYEKUTWA AMEFARIKI NYUMBANI KWAKE TAKRIBANI SIKU TANO,HUKU MLANGO UKIFUNGWA NA KUFULI KWA NJE
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,amefika kwenye Msiba wa Mwanamke Wande Kulwa mwenye Ualbino mkazi wa kijiji cha Nhelegani, aliyekutwa amefariki nyumbani kwake takribani siku tano,huku mlango ukifungwa na kufuli kwa nje.
Amefika kwenye Msiba huo leo Marchi 3,2025 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga.
Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa pole juu ya msiba huo na wameupokea kwa masikitiko makubwa, na kwamba wataendelea kushirikiana na familia ya marehemu,pamoja kuona nanma ya kulijengea kaburi lake.
"Poleni sana ndugu zangu kwa msiba huu,na kifo cha mwanamke huyu kina uwalakini licha ya kukutwa viungo vyake vipo, lakini utata unakuja nani alifunga kufuli kwa nje, hivyo kazi hii ya uchunguzi tunaliachia Jeshi la Polisi litakuja na majibu,"amesema Katambi.
"Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete nimempa taarifa juu ya tukio hili anawapa pole sana,na mimi nitawapatia mkono wa pole ili kusaidia mahitaji mbalimbali ya hapa msibani ikiwamo kununua chakula,"ameongeza Katambi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe,amesema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa, na kwamba tukio hilo limetokea katika mazingira ambayo siyo ya kawaida kwa kufungwa na kufuli nje ya mlango.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Manispaa ya Shinyanga Penina Ezekiel, amesema kifo cha mwenzao kimewapa mashaka,kuwa kipindi hiki cha uchaguzi maisha yao yapo hatarini.
Ameiomba serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama,kuwahakikishia usalama wao katika kipindi hiki cha uchaguzi, ili wasiuawe na kukatwa viungo vyao, huku akiomba kaburi la mwenzao lijengewe kwa ajili ya usalama zaidi lisije fukuliwa na kuchukuliwa viungo vyake.
Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya,amesema baada ya Polisi na Wataalamu kufanya uchunguzi katika mwili wa marehemu na kubaini hakuna kiungo kilichotolewa, waliukabidhi kwa familia na waliuzika majira ya saa 3 usiku hapo hapo nyumbani.
Baba wa mrehemu Mbiti Kulwa, amesema Mwanae alikuwa akiishi na Mama yake mzazi,lakini baada ya kuugua alimuacha na kuishi peke yake mpaka alipofariki.
Majirani wa mwanamke huyo,wanasema kifo chake kiligunduliwa na watoto ambao walikuwa wakichuma mboga, mara baada ya kusikia harufu kali ikitoka ndani pamoja na nzi,ndipo wakatoa taarifa kwa viongozi wa kijiji.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Kenedy Mgani,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini(kushoto)akimpa pole Baba mzazi wa marehemu mzee Mbiti Kulwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,akitoa salamu za pole.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Mkombe akitoa salamu za pole.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,akitoa salamu za pole.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464