PSSSF WAFUNGUKA MKUTANO WA MISA- TAN NA WADAU 2025

PSSSF WAFUNGUKA MKUTANO WA MISA- TAN NA WADAU 2025

Na Marco Maduhu,DODOMA

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (PSSSF) umeongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuboresha uwekezaji wake, na kufanikiwa kupandisha kiwango cha maendeleo kutoka asilimia 22 mwaka 2023 hadi asilimia 36 mwaka 2024/2025.
Lengo hili linakaribia asilimia 40 iliyopendekezwa kwa ajili ya kukuza uchumi wa Tanzania.

Hayo yamebainisha leo Machi 14,2025 na Mwanasheria Mkuu wa PSSSF Valentino Maganga, wakati wa wasilisho lake kwenye Mkutano Mkuu wa Wadau wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania Misa-Tan 2025.
Amesema mfuko huo wa hifadhi ya jamii alisema umefanikiwa kuongeza thamani ya uwekezaji kutoka trilioni 6 hadi trilioni 10, hatua ambayo inayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amesema kuwa jumla ya dhamana za uwekezaji zilizopo kwenye taasisi za kifedha, hususani benki na majumba, zinathamani ya Sh. Trilioni 9. dhamana ambazo zinachangia moja kwa moja katika kuongeza pato la taifa na maendeleo ya uchumi wa nchi.
Aidha, amesema PSSSF inalipa pensheni kwa wastafu kila mwezi kiasi cha Sh. Bilioni 70, na kwa mwaka ni zaidi ya Sh. Bilioni 800.

“Fedha hizi zinazolipwa kila mwezi zinachochea shughuli za uchumi na pia zinasaidia katika uwekezaji unaoingizia mapato Serikali,”amesema Maganga.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwanasheria Mkuu wa PSSSF Valentino Maganga akizungumza kwenye Mkutano wa MISA-TAN na wadau 2025.
Mwenyekiti wa MISA-TAN Edwin Soko akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano wa MISA-TAN na wadau 2025 ukiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464