BUTONDO AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI,AKABIDHI MAJIKO YA GESI KWA WAJASIRIAMALI KISHAPU


BUTONDO AMUUNGA MKONO RAIS SAMIA MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI,AKABIDHI MAJIKO YA GESI KWA WAJASIRIAMALI KISHAPU

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MBUNGE wa Kishapu Boniphace Butondo,amekabidhi majiko ya gesi kwa baadhi ya wajasiriamali jimboni kwake pamoja na watu weye Ualbino,ambao walimuomba awapatie majiko hayo, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia Nishati Safi ya kupikia,na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.
Amekabidhi majiko hayo jana katika Ofisi yake ya Mbunge wilayani Kishapu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi majiko hayo, amesema serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ipo kwenye mkakati kabambe wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na kuhamasisha wananchi watumie Nishati Safi ya kupikia, ili waondokane na matumizi ya mkaa na kuni, ambayo husababisha ukataji wa miti hivyo na kuharibu mazingira na hata kupoteza uoto wa asili.
“Naunga mkono juhudi za Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan dhidi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,ambapo nina leo nina kabidhi tena majiko ya gesi kwa wajasiriamali hawa na watu wenye Ualbino, ili waondokane na matumizi ya mkaa na kuni,”amesema Butondo.

“Awali nilishakabidhi tena majiko ya gesi 260 na nitaendelea kutoa tena, ni waombe tu wananchi wa Kishapu waondokane na matumizi ya mkaa na kuni, ili tutunze mazingira yetu,”ameongeza.
Diwani wa Kishapu Joel Ndettoson,amempongeza Mbunge huyo kwa kuendelea kufanya matukio makubwa ambayo yanaigusa jamii, na kwamba amekuwa ni Mbunge wa mfano ambaye amekuwa akitekeleza ahadi zake kwa vitendo.

Mmoja wa wajasiriamali ambaye ni Baba Lishe Masunga Kazi, amesema baada ya kupata jiko hilo la gesi, matumizi ya mkaa ndiyo “bye bye” kwake,na kueleza kwamba kwa siku moja alikuwa anatumia debe 3 za mkaa, na debe moja linauzwa kuanzia sh.9,000 hadi 10,000, tofauti na kujaza gesi ni sh,23,000 kwa mwezi.
Mjasiriamali mwingine Janety Philipo,amesema yeye anapotumia mkaa au kuni, moshi hua unamsumbua lakini kutokana na shida inabidi aendelee kutumia hivyo hivyo,na kumshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia majiko hayo ya gesi, na kumuomba aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wake.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi majiko ya gesi.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (kushoto)akikabidhi jiko la gesi kwa watu wenye Ualbino.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (wapili kutoka kulia)akibidhi jiko la gesi kwa mjasiriamali.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo (kushoto)akiendelea kukabidhi majiko ya gesi.
Mjasiriamali Janety Philipo akishukuru kupewa jiko la gesi na Mbunge Butondo.
Baba Lishe Masunga Kazi akishukuru kupewa jiko la gesi na Mbunge Butondo.
Picha za pamoja zikipigwa pamoja na majiko ya gesi.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa pamoja na majiko ya gesi.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa pamoja na majiko ya gesi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464