KATAMBI AKABIDHI COMBAT 100 KWA ITIFAKI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,amekabidhi Combat 100 kwa Itifaki ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Combat hizo zimekabidhiwa leo Machi 25,2025,na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson kwa niaba ya Mbunge Katambi.
Samweli amesema vijana hao walimuomba Mbunge Katambi awapatie Combat hizo kwa ajili ya shughuli za kichama, na kwamba leo amezikabidhi Rasmi,Combat 100 zenye thamani ya sh.milioni 3.5.
“Mbunge Katambi ameahidi kuendelea kushirikiana na umoja huu wa vijana UVCCM na leo amekabidhi maombi ya Combat 100 kwa Itifaki,”amesema Samweli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala,amemshukuru Mbunge Katambi kwa kutekeleza ombi lao, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana naye katika shughuli za kichama, na hata kukipatia ushindi Chama kwenye uchaguzi Mkuu 2025, wa kuchagua Madiwani,Wabunge na Rais.
TAZAMA PICHA👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Combat kwa Itifaki UVCCM.
Mwenyekiti wa UVCCM Abdulaziz Sakala akizungumza.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson (kulia) akikabidhi Combat za Itifaki kwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Sakala.
Muonekano wa Combat za Itifaki UVCCM ambazo zimetolewa na Mbunge Katambi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464