LEAT YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WA MAENDELEO JUU YA UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE NA ATHARI ZAKE


LEAT YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WA MAENDELEO JUU YA UCHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE NA ATHARI ZAKE

Na Marco Maduhu,DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wanasheria watetezi wa Mazingira (LEAT),kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari na wadau wa maendeleo kutoka taasisi zisizo za kiserikali,juu ya uchimbaji wa mkaa ya mawe na athari zake kwa jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Machi 28 Jijini Dar es salaamu.
Augustino Munuma.

Afisa Tathimini kutoka LEAT Augustino Munuma, amesema mafunzo hayo yamelenga dhidi ya kampeni ya uchimbaji makaa ya mawe, yenye kuzingatia afya za wananchi na utunzaji wa mazingira.

“LEAT ni marafiki wa Mazingira Tanzania, tulifanya utafiti juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe mkoani Ruvuma, na tumebaini kuna changamoto nyingi ambazo zinapaswa kufanyiwa kazi,likiwamo suala la utunzwaji wa mazingira na kujali afya za wananchi kutokana na utimuliwaji wa vumbi,”amesema Munuma.
Deodatus Mfugale.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale ambaye ni Mwandishi wa habari mwandamizi wa Mazingira,amewasisitiza waandishi wa habari, kwamba waandike zaidi habari za kuisaidia jamii kuliko kusifia sifia viongozi kila siku.

Amesema wananchi ambao wanaishi kwenye rasilimali za madini, wanahitaji kunufaika na rasilimali hizo na siyo kugeuka kuwa mateso kwao, na kwamba uwekezaji ni muhimu sababu unaongeza pato la taifa na ukuzaji wa uchumi,lakini ni vyema wawekezaji wakafuata sheria za nchi.
Nao baadhi ya waandishi wa habari,wamesema mafunzo hayo yamewajenga katika utekelezaji wa majukumu yao, na kuisaidia jamii ili wapate kunufaika na Rasilimali za nyumbani bila ya kuathiri afya zao na kuharibu mazingira.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464