RC MACHA AONGOZA DUA MAALUM YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA

RC MACHA AONGOZA DUA MAALUM YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA

Na. Paul Kasembo, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, ameongoza dua maalum ya kumuombea Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuwa na afya njema na kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Dua hiyo imefanyika jana nyumbani kwake,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini,vyama vya siasa,serikali na watoto wenye mahitaji maalum,ambapo ibada ilifanywa na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, mara baada ya Iftari.

Amesema dua hiyo ni maalumu kwa ajili ya kumuombea Rais Samia,aendelee kuwa na afya njema, nguvu, na ufanisi katika utendaji wake kazi wa kuwatumikia Watanzania, sababu ni Rais ambaye ndani ya utawala wake,amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo hapa nchini kwa muda mfupi.
“Dua hii ni muhimu kwa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan,aendelee kuwa na afya njema,kheri na Baraka,pamoja na maisha marefu,ili aendelee kuwatumikia Watanzania kwa ufanisi wa hali ya juu na kuwaletea maendeleo,”amesema Macha.

Aidha,Macha amewashukuru pia wafanyabiashara mkoani humo, kwa kutopandisha bei ya vyakula katika mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.
“Nawashukuru wafanyabiashara kwa kutekeleza ombi langu,hakukuwa na ongezeko la bei ya vyakula vya nafaka katika kipindi hiki cha mfungo,” amesema Macha.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza Ibada hiyo kumuombea Dua Rais Samia,amesema wanamuombea awe na afya njema,maisha marefu na yenye Baraka, ili aendelee kuwaongoza vyema Watanzania na kuwaletea maendeleo, na kwamba viongozi wa dini wapo pamoja naye kwa kila hatua.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza katika Dua ya kumuombea Rais Samia.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Mkusanya akiendesha Ibada katika dua ya kumuombea Rais Samia.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464