Kamwe sintosahau tukio hili katika mapenzi!
Naitwa Mage kutokea Kilosa, mimi na mpenzi wangu, tulidumu kwa zaidi ya miaka mitano ila hatukuwa na desturi ya kuonana mara mara kutokana na shughuli za kikazi ambazo zilituweka mbali kwa kiasi fulani.

Mara nyingi tulikutania kwake na kupata muda wetu hapo, wakati mwingine nililala hapo, sasa siku moja baada ya mizunguko yangu niliamua niende kwake nikapumzike maana nilikuwa najua sehemu anayoweka funguo.