Katambi afanya mikutano mikubwa Ndala na Masekelo
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,amefanya mikutano mikubwa Kata ya Ndala na Masekelo kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mikutano hiyo imefanyika jana Marchi 3,2025 kwa nyakati tofauti,ambapo Mbunge Katambi kwenye Mikutano hiyo ameambatana na Wataalamu kwa ajili ya kujibu kero za wananchi.
Katambi akizungumza na wananchi kwenye mikutano hiyo,amesema kwamba kero nyingi ambazo zilikuwa ni changamoto kwa wananchi nyingi amezitatua kwa kipindi cha miaka Minne ya Ubunge wake.
Amesema kwa upande wa elimu,miundombinu ya shule katika shule za msingi na secondari kwenye Kata hizo zimeboreshwa ikiwamo ukarabati wa vyoo,madwati pamoja na ujenzi wa madarasa.
Kwa upande wa maji,mtandao umesambazwa na wananchi wanapata majisafi na salama tofauti na miaka ya nyuma kabla hajawa mbunge, na bado wamepata fedha zingine za kupeleka maji zaidi kwa wananchi.
Amesema kwa upande wa miundombinu ya barabara nyingi zimekarabatiwa lakini baadhi ziliharibiwa na mvua,ambapo wamepata fedha na wanakwenda kuzikarabati upya,ikiwamo na ujenzi wa daraja jipya la upongoji.
Amezungumzia pia barabara ya kutoka Ndala kwenda Mwawaza kupita Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,kwamba fedha zimeshapatika za kuijenga kiwango cha lami na Zabuni yake imeshatangazwa,ili apatikane Mkandarasi na kuanza utekelezaji mara moja.
Kwa upande wa huduma za Afya,Zahanati imejengwa Masekelo na imeshaanza na kutoa huduma za matibabu kwa wananchi,pamoja kuboresha hospitali ya Rufaa,Kituo cha Afya Kambarage na ukarabati Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
"Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassani amefanya mambo makubwa kwenye Sekta ya Afya hapa Shinyanga na hospitali zetu zina vifaa tiba vya kisasa na madaktari, na hakuna tena kwenda Bugando wala Mubimbili matibabu yanapatikana hapa hapa,"amesema Katambi.
Amesema pia wananchi wengi wanahuduma za umeme, na waliosalia tayari kuma mradi mwingine unakuja na watafikiwa na huduma hiyo.
Aidha, akiwa Ndala amemuahidi kumpatia fedha sh.500,000 Bibi Ferister Mboyi ambaye hakuweza kuingizwa kwenye mpango wa TASAF, huku akiongezwe fedha nyingine na Diwani wa Ndala Zamda Shabani sh.250 000 na Afisa wa TASAF sh.50,000 na kufikisha sh.laki 8 ambazo atapatiwa kesho asubuhi.
Katika hatua nyingine Katambi amemuahidi kumpatia Kitimwendo mtoto Irene Julius ambay anatatizo la ulemavu wa miguu.
Katika mikutano hiyo ya hadhara wananchi walitoa kero zao,ikiwamo ya ubovu wa miundombinu ya barabara,ukosefu huduma ya umeme,migogoro ya ardhi,Tasaf na kulipishwa fedha za uzazi.
Mbunge Katambi kesho atahitisha ziara yake katika Kata ya Mwawaza na Chibe.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi,ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Diwani wa Ndala Zamda Shabani akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464