Kutoka kulipwa Sh30,000 hadi kumiliki Hoteli
Jina langu naitwa Salma mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, nimefanya kazi ya kupika na kuuza chakula hapa mjini kwa miaka 10 sasa tangu mume wangu alipoamua kuniacha na kuoa mwanamke mwingine.

Mume wangu aliponiacha nilipata hali ngumu ya maisha haswa kulipa kodi, kuwapatia watoto chakula, kuwavalisha na huduma nyingi ambazo wanastahili kupata.