BUTONDO ATEKELEZA AHADI YAKE AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI KISHAPU,AWASISITIZA WANAFUNZI WASOME KWA BIDII


BUTONDO ATEKELEZA AHADI YAKE AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA SEKONDARI KISHAPU,AWASISITIZA WANAFUNZI WASOME KWA BIDII

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ametekeleza ahadi yake na kukabidhi vifaa vya TEHAMA kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kishapu,ili kuunga mkono Juhudi za Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, za kuboresha sekta ya elimu, ili wanafunzi wasome na kupata ufaulu mzuri.
Ametoa vifaa hivyo leo Machi 22,2025 shuleni hapo, na kuwakabidhi wanafunzi pamoja na Mkuu wa shule hiyo Buhoro Mipawa.

Butondo akikabidhi vifaa hivyo,amesema yeye akiahidi hua anatekeleza,ambapo aliwahidi wanafunzi hao kuwapelekea vifaa hivyo vya TEHAMA pamoja na Televission kwa ajili ya kuangalia taarifa ya habari hasa kwa siku za "weeckend", na sasa ametekeleza.
“Leo nimetekeleza ahadi yangu kwenu na kuwaletea vifaa hivi vya TEHAMA, ambavyo ni Printer, Moniter Screen,CPU, Projector, pamoja na Television ambayo mliniomba kwa ajili ya kuangalia Taarifa ya habari,”amesema Butondo.

“Vifaa hivi vitawasaidia pia Walimu katika maandalizi ya masomo pamoja na kuchapa Mitihani,hakuna tena kwenda kwenye Stationary za watu binafsi, pia itapunguza na gharama za uaandaaji wa mitihani,”ameongeza.
Aidha,ameomba vifaa hivyo vitunzwe pamoja na kutumiwa vizuri ili vidumu kwa muda mrefu, huku akiwasisitiza wanafunzi wasome kwa bidi ili watimize ndoto zao.

Diwani wa Kishapu Joel Ndettoson, amempongeza Mbunge Butondo kwa kutekeleza ahadi zake,na kutoa vifaa hivyo vya TEHAMA shuleni hapo,huku akiahidi kumuunga mkono kwa kununua kifurushi kila mwezi ili wanafunzi hao wawe wanaangalia taarifa ya habari na kuona mambo makubwa ambayo ya maendeleo ambayo anayafanya Rais Samia.
Mkuu wa shule hiyo Buhoro Mipawa, amemshukuru Mbunge Butondo kwa vifaa hivyo vya TEHAMA, kuwa amevitoa katika muda muafaka ambapo dunia ya sasa ipo kwenye ulimwengu wa Sayansi na Tecknolojia, na kwamba vifaa hivyo vitaongeza ubora wa taaluma shuleni hapo.

“shule yetu hii imekuwa ikifanya vizuri katika taaluma na tunamshukuru Mbunge kwa kutuletea vifaa hivi vya TEHAMA, mfano kwa matokeo ya mwaka 2024 ya kidato cha 4, ambapo wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 94, daraja la kwanza walipata 4, la pili 19, tatu 40 na daraja la 4 walikuwa 31,”amesema Buhoro.
“Matokeo ya kidato cha Sita 2024 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 67, waliopata daraja la kwanza walikuwa 57, daraja la pili 10, hakuna aliyepata daraja la 3 wala 4,”ameongeza.

Nao baadhi ya wanafunzi, wamemshukuru Mbunge Butondo kwa kutekeleza ahadi yake kwao, huku wakimuahidi watasoma kwa bidii.

Butondo mbali na kutoa vifaa hivyo vya TEHAMA kwa wanafunzi hao, pia aliwapatia mchele kwa ajili ya kula chakula cha jioni na kubadilisha mlo.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Vifaa vya TEHAMA Shule ya Sekondari Kishapu.
Diwani wa Kishapu Joel Ndettosn akizungumza.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Fadhili Mvanga akizungumza.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benson Werema akizungumza.
Mkuu wa shule ya Sekondari Kishapu Buhoro Mipawa akizungumza .
Meza kuu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi Vifaa vya TEHAMA.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akikabidhi Vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari Kishapu.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akikabidhi Mchele.
Awali Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akivalishwa Skafu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464