KATAMBI KUMTIBU KIJANA ALIYEPOFUKA MACHO UKUBWANI,AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KATA KWA KATA


Kijana aliyepofuka macho ukubwani Shija Barabara

Katambi kumtibu kijana aliyepofuka macho ukubwani,ahitimisha ziara yake ya Kata kwa Kata

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,amehitimisha ziara yake ya Kata kwa Kata,huku akiahidi kumsaidia matibabu kijana Shija Barabara mkazi wa Mwawaza ambaye alipofuka macho ukubwani.
Katambi amehitimisha ziara yake leo Machi 4,2025 kwa kufanya kikao na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Mwawaza na Chibe pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye Kata hizo.

Akiwa Mwawaza akipokea kero mbalimbali za wananchi,aliguswa na kijana Shija Barabara ambaye alipofuka macho mwezi wa 9 mwaka jana, ambaye alimuomba msaada na kuamua kumsaidia tatizo lake hilo ili arudi katika hali ya kawaida.
Amesema kwa vile tatizo hilo limemtokea ukubwani,huenda kunashida ndogo ambayo imejitokeza kwake, hadi kusababisha kutoona tena, hivyo atampeleka hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,kufanyiwa vipimo upya ili kubaini tatizo ni nini,na kuanza kupatiwa matibabu.

"Nimefurahishwa na taaluma yako ya nyimbo za Jadi,ninakupa Ofa ya kurekodi nyimbo hizo ambapo gharama zote zitakuwa juu yangu,na pia kama upo tayari hata leo nitakuchukua au kesho ili uwaage ndugu zako nitakupeleka pale hospitali ya mkoa upate vipimo ili kubaini tatizo lako la macho na upate kuona tena,"amesema Katambi.
Aidha,Katambi akizungumzia suala la maendeleo kwenye Kata hizo mbili Mwawaza na Chibe, kwamba wameboresha huduma kwenye Sekta za Afya ikiwamo ujenzi wa Zahanati,Miundombinu ya Elimu,Maji,Umeme,na kwamba kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hizo kuna miradi bado inaendelea kutekelezwa.

Diwani wa Mwawaza Juma Nkwambi,akizungumza kwenye Mkutano,amemshukuru Katambi kwa kuchangiza masuala ya maendeleo kwenye Kata hiyo chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Diwani wa Chibe Peter Kisandu,amesema Chibe ya sasa siyo ya zamani,ambapo imepiga hatua kubwa kimaendeleo,kwa kupiganiwa na Mbunge Katambi.

Nao baadhi ya wananchi kwenye Kata hizo walilalamikia ubovu wa barabara,ukosefu wa maji,umeme pamoja na migogoro ya ardhi,ambapi pia wataalamu walioambatana na Mbunge walijibu kero hizo.

Aidha,Katambi akiwa Chibe Wazee wa Kimila kwenye Kata hiyo alimpongeza kwa kazi anayofanya ya kuwatumikia wananchi na kisha kumbariki Kijadi na kumpatia jina la "Ngw'ijigijiwa"

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu akizungumza na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu,akisimikwa na wazee wa Chibe na kupewa jina la Ng'wijigijiwa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464