SHUWASA WAADHIMISHA WIKI YA MAJI NA WADAU WATEMBELEA KUONA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MAJI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)imeadhimisha wiki ya maji na wadau, kwa kutembelea kuona shughuli za uzalishaji maji hadi kumfikia mteja.
Ziara hiyo imefanyika leo Machi 19,2025 kwa kutembelea chanzo cha Maji Bwawa la Ning’hwa,Mtambo wa kutibu Maji, Tangi la kuhifadhia Maji ya Ziwa Victoria Oldshinyanga, pamoja na kuona mtambo wa kuchakata tope kinyesi.
Afisa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka SHUWASA Nsianel Gerald, amesema wameadhimisha wiki ya maji, kwa kuwatembeza wadau wao kuona shughuli ambazo hua wanazifanya za uzalishaji maji hadi kumfikia mteja, ili wawe Mabalozi wazuri wa Shuwasa.
“Tumetembelea chanzo cha maji katika Bwawa la Ning’hwa,Mtambo wa kutibu maji, Tangi la kuhifadhia maji ya Ziwa Victoria Oldshinyanga, pamoja na Mtambo wa kutibu tope kinyesi,”amesema Nsianel.
Nao wadau hao akiwamo Adamu Mbega,amesema baada ya kuona shughuli hizo, wamewapongeza SHUWASA kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya, huku akitumia fursa hiyo kuwaomba wateja wa Shuwasa wawe wanalipa billi kwa wakati, akieleza kwamba kazi ya kuzalisha maji hadi kumfikia mteja ni gharama kubwa.
Naye Rehema Kailani,amewaomba wananchi kwamba waitunze miundombinu ya maji pamoja na vyanzo vya maji, sababu uwekezaji uliofanyika ni gharama kubwa, huku akiwashukuru Shuwasa kwa kuwatembeza kuona hatua zote za uzalishaji maji hadi kumfikia mteja.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya maji 2025 inasema”Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa uhakika wa maji”
TAZAMA PICHA👇👇
Afisa Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka SHUWASA Nsianel Gerald akizungumza katika ziara hiyo.
Mdau wa Maji Adamu Mbega akizungumzia ziara hiyo.
Mdau wa Maji Rehema Kailani akielezea ziara hiyo.
Wadau wa maji kutoka SHUWASA wakiwa kwenye Chanzo cha Maji Bwawa la Ning’hwa.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye mtambo wa kutibu Maji kabla ya kusambazwa kwa wateja.
Wadau wa maji wakiwa kwenye Tangi la Maji ya Ziwa Victoria Oldshinyanga.
Wadau wa maji wakiwa kwenye mtambo wa kutibu tope kinyesi.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464