TASAF WAELEZA MAFANIKIO MKUTANO WA MISA-TAN NA WADAU “SUMMIT”2025

TASAF WAELEZA MAFANIKIO,MKUTANO WA MISA-TAN NA WADAU “SUMMIT”2025

Na Marco Maduhu,DODOMA

MRATIBU wa malipo ya kielektroniki kutoka mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), Josephine Joseph, amesema mpango wa uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini umeleta mafanikio makubwa hasa katika sekta ya elimu.
Amebainisha hayo leo Machi 14,2025 kwenye Mkutano wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania MISA-TAN 2025 Jijini Dodoma.

Amesema kupitia mfuko huo wa TASAF watoto wa kaya maskini wanapata fursa ya kusoma hadi vyuo vikuu, na hadi sasa, mtoto mmoja amemaliza stashahada yake mwaka 2024.
“Watoto wengi kutoka kwenye kaya maskini wamefaulu masomo yao ya darasa la saba na sekondari, na wengine wameweza kujiunga hadi vyuo vikuu,”amesema Josephine.

Aidha, Joseph alifafanua kuwa TASAF imefanikiwa kufanya mazungumzo na bodi ya mikopo, na sasa watoto wa kaya maskini wanapata mikopo ya asilimia 100 kwa ajili ya masomo yao hali ambayo imewezesha wengi kumaliza masomo yao kwa urahisi zaidi.

“Nawashukuru waandishi wa habari kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya juu ya mfuko huu wa TASAF,”ameongeza.

TAZAMA PICHA👇👇
Mratibu wa malipo ya kielektroniki kutoka mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF), Josephine Joseph akizungumza kwenye mkutano wa MISA-TAN na wadau "SUMMIT" 2025.
Mwenyekiti wa MISA-TAN Edwini Soko akizungumza kwenye mkutano wa MISA-TAN na wadau SUMMIT 2025.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464