TAMASHA KUBWA LA MICHEZO YA JADI KUFANYIKA SHINYANGA
TAMASHA kubwa la Michezo ya Jadi linatarajiwa kufanyika mkoani Shinyanga, ili kudumisha Mila na Tamaduni za Mtanzania.
Hayo yamebainishwa leo Machi 24,2025 na Mratibu wa Chama Cha Michezo ya Jadi Taifa(CHAMIJATA)Abubakary Kyaibamba, wakati wa kikao na viongozi wa ngazi ya wilaya wa Chama hicho mkoani Shinyanga.
Amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anadumisha masuala ya utamaduni, na kwamba siku ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26 mwaka huu,amesisitiza watu wa utamaduni wawepo kwenye maadhimisho hayo Jijini Dodoma,na kabla ya hapo wao watafanya kwanza Tamasha kubwa la Michezo ya Jadi mkoani Shinyanga Aprili 12,2025.
“Rais Samia ni muumini sana wa masuala ya utamaduni, na ndiyo maana alicheza na Filamu ya Royar Tour na hata kushiriki mambo ya kimila na kupewa jina la Chifu Hangaya, na amesisitiza Michezo ya Jadi ifufuliwe na kuenziwa,”amesema Kyaibamba.
Amesema, michezo hiyo ya Jadi iliasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1971,kwa lengo la kulinda Utamaduni wa Mtanzania ili watu wasipoteze asili yao.
“Michezo ya Jadi ni kurudisha Utamaduni wa Mtanzania, na Taifa lisilo na Utamaduni limepoteza asili yake, Michezo hii pia ni kielelezo cha Taifa na Urithi wetu,”amesema Kyaibamba.
Aidha,amesema michezo hiyo ya Jadi ni ajira, na pia anaingiza kipato na hata kuwatoa vijana kwenye makundi mabaya ikiwamo kuvuta bangi na kushinda kwenye Kamari “Beating” na kutolea mfano mchezo wa mbina “ngoma za Jadi”ni utambulisho mzuri wa mkoa wa Shinyanga na hata kuvutia watalii.
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga Janety Elias,amesema michezo hiyo ya Jadi ni kuenzi Mila na Desturi za Mtanzania, na hata kurudisha maadili yetu, na kwamba serikali ya mkoa huo itaendelea kushirikiana na Chama hicho cha Michezo ya Jadi.
Kauli mbiu ya Chama hicho inasema”Michezo ya Jadi ni kielelezo cha Taifa na Urithi wetu.
TAZAMA PICHA 👇👇
Mratibu wa Chama Cha Michezo ya Jadi Taifa (CHAMIJATA)Abubakary Kyaibamba,akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Michezo ya Jadi Mkoa wa Shinyanga Isaya Meru,akizungumza kwenye kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Michezo ya Jadi Mkoa wa Shinyanga Frida Malleko,akizungumza kwenye kikao.
Katibu wa Chama Cha Michezo ya Jadi Tabea Chepe,akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Habari wa Chama Cha Michezo ya Jadi Mkoa wa Shinyanga Nyamiti Alphonce,akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga Janety Elias akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao Chama Cha Michezo ya Jadi kikiendelea mkoani Shinyanga.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464