Wasira aonya wanaotaka kununua Ubunge,awashauri wafungue maduka
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara Stephen Wasira amewaonya wanaotaka kununu nafasi za ubunge kwamba kufanya hivyo ni ukiukaji wa maadili ya Chama na watachukuliwa hatua,huku akiwashauri fedha zao ni vyema wakafungua maduka.
Amebainisha hayo leo Machi 26,2025 wakati akizungumza na WanaCCM, pamoja na Makundi mbalimbali ya watu,mkutano uliofanyika Mjini Shinyanga.
Amesema Chama hicho kimebadilisha mfumo wa wagombea kuchaguliwa kwa kura za maoni,ambapo wajumbe wameongezeka kutoka 400 hadi 4,800 kwa lengo la kupata Mgombea Ubunge ambaye anatokana na chaguo la watu.
"Zamani mlikuwa mkiwahonga sh.Laki moja moja wajumbe hao 400,sasa hivi wapo 4,800 kwa sh.hiyo laki moja sawa na milioni 400 si bora fedha hizo ufungue duka, unanunua Ubunge wa nini na wakati mshahara wa Mbunge ni Sh.milioni 4,"amesema Wasira.
"kwa kiasi hicho cha fedha sh.milioni 400 huwezi kutoa utawapa tu sh.elfu 10 na sisi tunakushughulikia kimaadili tunataka mtu achaguliwe kwa hiari ya wapiga kura na siyo kununua Ubunge,lazima turudishe nidhamu ya Chama,"ameongeza.
Aidha,amewataka wana CCM kuwapuuza baadhi ya watu ambao wamekuwa akibeza kwamba serikali chini ya CCM ndani ya miaka 60 haijafanya kitu.
Amesema ndani ya miaka hiyo 60 ya CCM,nchi imepiga hatua kubwa kimaendeleo ikiwamo ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati.
"Rais ambaye yupo Madarakani kwa sasa Dk.Samia Suluhu Hassan kipindi ana achiwa nchi hii na hayati Rais John Pombe Magufuli baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi naye, sasa ni waulize tu maendeleo mnayaona hamuyaoni....tunayaona,"amesema Wasira.
Watu walipiga kelele suala la Bandari, sasa hivi badari yetu ni mshindani mkubwa kwa soko sababu ufanisi wake, pia bwawa la Mwalimu Nyerere limekamiika kwa asilimia 100,pamoja na Daraja la Magufuli pale Busisi mwezi ujao linafunguliwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amemshukuru Rais Samia kwa kuutendea haki mkoa huo kwamba ametoa fedha nyingi na miradi ya maendeleo imetekelezwa.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amesema jimbo hilo chini ya Rais Samia limebadilika kimaendeleo ukiwamo na ujenzi wa Uwanja wa Ndege,miundombinu ya barabara,madaraja,sekta ya elimu,Afya.
Aidha,katika Mkutano huo Wasiria alifanyiwa masuala ya kimila na kupewa jina la KilelaMhina likiwa na cheo cha Namhala Ntale.
Stephen Wasira kesho ataendelea na ziara yake wilayani Kahama.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira akizungumza kwenye mkutano.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye mkutano.

Wazee wakimfanyia masuala ya Kimila Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira na kumpatia jina la Kilela Mhina lenye cheo cha Namhala Ntale.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464