NYAKANYENGE ASHINDA TENA UMWENYEKITI CWT USHETU AWABWAGA WAPINZANI WAKE

Neema Sawaka,Kahama

CHAMA cha Walimu  Wilaya ya Ushetu  Mkoani Shinyanga  kimefanya uchaguzi nakumchagua Juma Nyakanyenge kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa  mara nyingine baada ya kumshinda  mpinzani wake  Petro Basili.

Katibu wa  CWT  Mkoa wa Shinyanga  Kizito  Shuli  ametangaza matokeo hayo leo tarehe 24/03/2025  baada ya kufanya  uchaguzi  katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi  nakuhudhuliwa na wajumbe  zaidi ya 140   ambapo Nyakanyenge alipata kura  78 huku mpinzani wake akipata kura 68 na kura moja iliharibika.

Shuli aliendelea kutangaza  matokeo ya nafasi ya Mwekahazina   alishinda  Wambura Yudas  aliyerudia nafasi hiyo kwa mara nyingine   huku akiwashinda wapinzani wake  wawili ambao ni  Ally Nurali  na Frank Zoto  

Pia ameendelea kutaja Kundi la uwakilishi  walimu vijana aliyeshinda ni  Mwalimu  Johanes Samweli  na kundi la uwakilishi walimu wanawake aliyeshinda ni   Mwalimu Ana Nzingu.

Mwalimu Said Soja  alipata  nafasi ya uwakilishi wa   walimu wenye ulemavu  kwa kupigiwa kura za ndiyo na hapana ambapo  alipata  kura 139  za ndiyo huku kura  tano  zikizema  hapana ambapo kinyang’anyiro hicho alikuwa hana mpinzani .

Baada ya kutangaza matokeo hayo Katibu Shuli amesema matokeo  yaliyopatikana wayakubali nakuvunja makundi waliyokuwa nayo  nakutakiwa kuwa wamoja.

Mwenyekiti   Nyakanyenge wakati akitoa shukrani  kwa wajumbe amesema sasa kazi imeanza ataendelea kutoa ushirikiano aliokuwa nao zamani  kuhakikisha haki na maslahi ya walimu vinaendelea kuwepo.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464