UBEBAJI MIMBA UNATEGEMEA WAZAZI KUANZA MAANDALIZI YA AFYA BORA ILI KUMJENGA MTOTO

Na Kareny  Masasy, Msalala

WANAWAKE  wengi wamekuwa hawafuati utaratibu wa kiafya ikiwemo lishe bora huku wakitarajia  kubeba ujauzito na  kutegemea kupata mtoto mwenye akili hilo litakuwa suala gumu.

Hayo yamesemwa tarehe 5, March,2025  na Afisa elimu  Afya  kutoka  halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Peter Ngazo kwenye kongamano la wanawake  lililofanyika kata ya Bugarama.

Ngazo amesema  wazazi wengi wamekuwa wakidai  mimba walizobeba niza bahati mbaya  matokeo yake wanapoanza kuzilea mimba hizo huku mtoto akiendelea kukua  tumboni anaendelea mama naye anakuwa akila   udongo wa pemba.

“Mtu anayekuwa udongo wa pemba huyo anaupungufu wa madini ya zinc  ambayo yanapatikana kwenye mboga za majani ambapo mboga hizo za majani kama mchicha  watu wamekuwa wakidharau nakuona kama hauna faida mwilini angalau angekuwa nyama”anasema Ngazo.

Ngazo amesema utafiti umeonyesha  wanawake wenye umri wa kuzaa  wamekuwa wakibeba mimba kabla ya kujiandaa  ndiyo maana matatizo   yamekuwa yakitoke kwa kupatwa na hali  ya upunguvu wa madini mwilini  na waelewe  changamoto hiyo ndiyo inayowafanya  kuzaa watoto wenye changamoto.

Ngazo amesema  serikali imejenga vituo  vya afya kila kona  ni wajibu wa wazazi kwenda kupima afya zao kabla ya kubeba mimba ili wajiandae na malezi ya mtoto kuanzia tumboni nakuondokana na ulaji wa udongo wa pemba ambao unasababishwa na kukosa madini  chuma mwilini.

“Utakuta  mjamzito haendi kliniki mpaka mimba ifikishe umri wa miezi saba au nane hajui maendeleo ya mtoto aliyeko tumboni wakati mwingine anazalia nyumbani hapo unategemea utaleta kiumbe chenye utimamu wa akili  duniani kweli”amesema Ngazo

Ngazo amesema wanawake wanategemewa kuwa madaktari namba moja  kwa kujua hali ya mtoto kabla ya kuzaliwa  daktari hospitalini yeye wa pili kukuelekeza  wakifanya hivyo wataweza kuokoa vifo vya watoto na kuondoa changamoto zingine zenye kuzuilika.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464