WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO NI HATARI KWA UGONJWA WA MALARIA


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga,Anamringi Macha akizindua kampeniya ugawaji wa  vyandarua ngazi ya Kaya  mkoani Shinyanga februari,2025 na kutoa ujumbe jamii  wa kulinda afya za watoto dhidi ya malaria.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga ,Anamringi Macha akizindua kampeniya ugawaji wa  vyandarua ngazi ya Kaya  mkoani Shinyanga februari,2025

Na Kareny Masasy.
Hali ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2025 – Kwa Mujibu wa WHO

Kwa mujibu wa ripoti ya World Malaria Report 2024 iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), malaria bado ni tatizo kubwa la kiafya duniani, hasa barani Afrika. Mnamo mwaka 2023, kulikuwa na takriban visa milioni 263 vya malaria duniani, ongezeko la visa milioni 11 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Vifo vilivyokadiriwa vilifikia 597,000, ambapo asilimia 94 ya visa na asilimia 95 ya vifo vilitokea katika Kanda ya Afrika ya WHO, na asilimia 76 ya vifo hivyo vilikuwa miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5

​Kila mwaka aprili 23, ni siku ya malaria duniani,Mwaka huu Kaulimbiu ya malari  ni "Malaria Inaisha na Sisi: Wekeza Tena, Fikiria Upya, Chochea Upya", ikihimiza jamii ya kimataifa kuongeza uwekezaji na kubuni mbinu mpya za kukabiliana na malaria kwa ufanisi zaidi

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Mkoa wa Shinyanga unakabiliwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria. Kwa mwaka 2023, Shinyanga iliorodheshwa kuwa mkoa wa nne kwa maambukizi ya juu ya malaria nchini, ikiwa na kiwango cha maambukizi cha asilimia 16. Hii ni juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 8 .

Kauli za Viongozi wa Mkoa wa Shinyanga Kuhusu Malaria (2025)


Mkoa wa Shinyanga unaendelea kupambana na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria, ambacho kwa sasa kimefikia asilimia 16, na kuwa mkoa wa nne kwa maambukizi nchini. Viongozi wa mkoa wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa kauli na kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na hali hii.

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga – Mhe. Anamringi Macha

Mhe. Macha alizindua rasmi kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa kaya zote mkoani Shinyanga mnamo Februari 2025, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika kupambana na malaria. 

"Mkoa wa Shinyanga ni wa nne kitaifa kwa maambukizi ya malaria, ambapo kiwango cha kitaifa cha maambukizi ni asilimia 8.1. Tunahitaji ushirikiano wa kila mmoja ili kupunguza maambukizi haya." alisema​

 Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga – Bi. Bety Shayo

Bi. Shayo alieleza hayo februari 2025, kuwa zaidi ya vyandarua milioni 1.5 viligawiwa kwa wakazi wa mkoa huo, kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, TAMISEMI, na Bohari Kuu ya Dawa, kwa ufadhili wa Global Fund. ​

"Ni muhimu kwa wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa usahihi ili kufikia lengo la kutokomeza malaria mkoani Shinyanga."alisisitiza:

  Mikakati ya Kupambana na Malaria

Ukweli ni kwamba,Serikali ya Tanzania imechukua hatua madhubuti kupambana na malaria katika mkoa wa Shinyanga. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na Usambazaji wa vyandarua vyenye dawa

 Hata hivyo, serikali ilianza kusambaza vyandarua milioni 1.5 kwa kaya zote zilizosajiliwa katika mkoa wa Shinyanga.

Usambazaji huo ulikuwa na Lengo la kupunguza maambukizi ikiwa  Mpango wa maendeleo wa mkoa ulilenga kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9.7 ifikapo Juni 2024, lakini juhudu zinatakiwa kuongezeka  ilikufikia  asilimia 7 ifikapo Juni 2027.

Sababu Zinazochangia Maambukizi

Watalam wamebainisha kuwa maambukizi ya malaria yanaathiriwa na sababu mbalimbali, zikiwemo:​Mazingira ya kijiografia yenye mazalia ya mbu yanaongeza hatari zaidi ya maambukizi.

Pia upatikanaji mdogo wa huduma bora za afya unaweza kuchelewesha utambuzi na matibabu ya malaria kwa mtu mwenye dalili

Sabubu zingine zinaelezwa ni  uelewa mdogo kuhusu njia za kujikinga na malaria na  kuweza kuchangia kuenea kwa ugonjwa huu. 

Ushauri kwa Wakazi wa Shinyanga

Ili kujikinga na malaria, inashauriwa kuendelea kutumia vyandarua vyenye dawa kila usiku,Kufika vituo vya afya mapema pindi unapohisi dalili za malaria kama vile homa, kutetemeka, maumivu ya kichwa, na uchovu,kushiriki katika kampeni za usafi wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu na kuelimishana ndani ya jamii kuhusu njia za kujikinga na malaria.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464