Madhara ya kutembea na mke wa mtu!
Niliishi karibu na jirani yangu Kim ambaye alikuwa pia ni rafiki wangu wa dhati kwani alinisaidia mambo mengi maishani. Urafiki ule ulikuwa wenye kutamaniwa na wengi kwani hata watu wengi walisema kuwa tulikua mashoga lakini hiyo ilikuwa ni propaganda isiyo na msingi wowote.

Siku ziliposonga, Kim alifanikiwa kupata jiko na hapo ikawa urafiki wangu na wake ukaanza kudidimia kwa kuwa wakati mwingi alitumia kukaa na mke wake.